UKWELI HUMUACHA MTU HURU,,,
Unapoamua kuingia kwenye mahusiano jitahidi sana kua mkweli,siku zote mapenzi ya kweli hua hayachagui,kua mkweli tuu kwa mwenza wako hata kama unalala chini muelezee tuu kama ameshaamua kukupenda hatolijali hilo,
haina haja yakuazima chumba cha mshkaji wako ukijiachia eti na kujiona upo juu huo ni uboya,kama hauna hata baiskeli kua mkweli tuu we mwambie sina ata baskeli lkn nimekupenda,
kama ameamua kukupenda hatolijali hilo lkn unapoazima gari la rafiki yako kumbuka njia ya muongo fupi,kuna haja gani yakujisumbua akili kwa vitu vya kuazima?pambana na hali yako,,
Itakua siku zote unatumia njia za udanganyifu ili kuwapata kina mwajuma,na unawapata kweli kwa kua nia yao ni kutaka mwanaume anaeonekana anazo,lkn kuna siku utajikuta unaangukia kwa mwanamke mwenye akili zake timamu,mwenye msimamo wake,ambae alijitolea tuu kukupenda vyovyote ulivyo lkn akigundua uongo wako anakuacha mchana peupee,,
Pambana na hali yako
Mwambie tuu ukweli,usifiche ata kama unalalia mkeka we mwambie tuu pengine ujio wake ndio utakaokufanya ukapata baraka ata kuambulia kupata godoro ili muanze maisha
Pambana na hali yako
Uongo haukusaidii kitu na njia ya muongo fupi siku zote,ukweli hukuacha huru na kuishi kwa amani
Lkn ukiishi kwa uongo huwezi kua huru,huwezi kua na amani,utaishi kwa kujificha ficha ili kuficha aibu yako
Mwanamke akiamua kukupenda hata ukimwambia unalala kwenye duka likishafungwa mie naamini mtalala pamoja kama walinzi mpaka mtapofanikiwa kupata chumba chenu,lkn ukitumia uongo utajikuta kuna siku unaipoteza lulu iliyokuja kumulika maisha yako bila ya kutegemea
Pambana na hali yako
Thursday, July 13, 2017
UKWELI HUMUACHA MTU HURU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Fish balls
FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...
-
Pishi hili maarufu kama Sphagetti bolognese,ni mchanganyiko wa tambi,nyama ya kusaga na njegere(optional). MAHITAJI: 1. Tambi mfuko mmoja...
-
#biriani #goatbiriani #beefbiriani #birianiyambuzi Mahitaji 1.Mchele wa Basmat 1/2 Kg 2.Nyama ya Mbuzi Stake 1/2 Kg 3.Viazi mbatata viku...
-
Jinsi ya kutengeneza lipbam Aina ya kwanza mahitaji Vaseline /mafuta yoyote ya mgando yani petroleum jelly Mafuta ya Nazi Asali Rangi ...
No comments:
Post a Comment