Tuesday, August 29, 2017

KUA TOFAUTI

Usiogope kujaribu ikiwa kama haivunji utu wako.

Usiogope kujifunza hata kama umechoka

Usiwe kama wale wanaoweza kuwasema wengine vibaya nyuma ya pazia wana makosa mazito zaidi yao

Usiwe kama wale wasiomuamini  Mungu,


Usiwe kama wale ambao hawajui ukarimu na Upendo na heshima.

usiogope kukosea, kwani ndio njia sahihi ya kujifunza

Usiache kutenda wema hata kama una sababu ya kutomuamini tena



Usiogope  kushirikiana nao ata kama wanakubeza

Usiache kumshukuru Mungu kwa magumu na mepesi.

Usiishi pia kwa kuangalia mabaya tu, ukumbuke na  mema pia


Friday, August 18, 2017

UWAZI NA UKWELI



Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano(UWAZI NA UKWELI)

Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo Na Ukamilifu,

Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye


Jinsi Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua. Kuendelea Na Migogoro Isiyosuluhishwa Husababisha Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako.


Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa Kutoka Ili Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku Na Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa Kuwa Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka..


Monday, August 14, 2017

MAMBO MATANO YAKUZINGATIA KIAFYA

Naomba nikujuze mambo matano muhimu yakuimarisha afya yako ila kumbuka awali ya yote mazoezi ni muhimu kwa afya yako.


1. unaishi sehemu yenye baridi kali unataka uhisi joto? lamba asali kijiko kimoja halafu unaweza ukachemsha tangawizi ukanywa, tumai muda mwingi tumia kusugua viganja vyako vya mikono na uviweke mashavuni.


2. Unahisi maumivu ya viungo? miguu, mikono, mgongo n.k? chemsha bamia bila chumvi kunywa, pia pendelea kula kijiko kimoja cha asali kilichochanganywa na mdalasini


3. Kichwa kinauma sana? kata ndimu kipande na ujisugue paji la uso, kunywa maji kwa wingi,chemsha chai ya rangi yenye majani mengi kunywa na kwa wadada epuka kuvaa vilemba vyeusi kichwani

.
4. Una tatizo la kusahausahau? pendelea kunywa juice ya mabungo, chemsha bilinganya tia tangawizi, nyanya, kitunguu na chumvi kidogo kula kama mboga,hii pia ni nzuri kwa wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo.


5.Unamatatizo yakusinzia mara kwa mara? chemsha kahawa tia iliki na rose water kidogo sana, kunywa kutwa mara tatu, hii pia ni nzuri kwa vile inatibu maradhi ya ini na figo na kwa wale madj, na wafanyakazi waendao shift ya usiku ni nzuri pia, natumai umenielewa,


jitahidi kutenga muda kwa ajili ya kulala ili kuipumzisha akili japo masaa mawili kwa mchana kwa wale wasio na kazi,na kwa waendao makazini basi hakikisha usiku unalala si chini ya masaa manane,


UPISHI WA MAKORONYA

MAKARONI

mahitaji

makaroni pacti  (1)

tomato fresh  (4-5)

kitunguu maji (1-2)

hoho (1)

karoti  (1)

maji ya moto kiasi

nyama nusu

mafuta yakupikia kiasi

chumvi kiasi

tomato pest (1)

ndio au limao (2-3)

NAMANA YA KUFANYA

marinet nyama na vitu vyako

katakata vitu vyako vyoo te na Anza kukaanga kama unavyotaka kupika mchuzi Tia chumvi pia Tia na tomatopest

kisha tia nyama yako ipikie mle huku unageuza iachie kidogo

chukua sufuria injika jikoni maji yakichemka weka makaron yako na mafuta kidogo  na chumvi funika acha ichemke

tizama nyama yako kama tayari Tia ndim onja acha kidogo

makaroni yako ukiona yameisha (yamelainika) yachuje na kisha yatie kwenye nyama yako

halafu geuza geuza acha yachemke kidogo halafu ipua

mimina kwenye chombo chako halafu weka mezani ita family yako muenjoy


Sunday, August 13, 2017

AINA ZA WANAWAKE WASIOFAA KUWATEGEMEA

MWANAMKE ANAWEZA KUWA SEHEMU KUBWA YA MAFANIKIO YA MWANAUME.

Kuna kauli unaijua

Behind every successful man there is a great woman.

Sasa sio wanawake wote wanaweza kumfanya mwanaume afanikiwe.

Mungu aliumba mwanamke awe msaidizi. Kuna wanawake sio wasaidizi wala hawawezi kabisa mambo hayo wanaamini haki sawa, ila ulete hela wewe. Zako zenu, zake zakwake mwenyewe.
Haiwezekani uwe successful huku kichwa cha familia vinashindana na mkono, moyo, miguu, hamuwi mwili mmoja tena.

IKIWA mwanamke wako kalala na mwanaume mwingine atasaidia kujenga falme ngapi. Lazima Moja ataibomoa, successful man wanawake wao hutowasikia kwenye skendo yoyote ya kulala na wanaume zaidi ya wanaume wao, mfano. Michele Obama, Jacqueline Meng, Nancy Sumari, Zari

Na haimaanishi wanaume wao hawakosei, wanaweza kukosea, ila wanawake hawa wanajua wakidanga (kuchepuka) watavunja ufalme wa waume zao.

Mwanamke atayekufanya uwe successful ataona uwezo wako wa kujenga ufalme, ataona udhaifu wako, atakutunzia heshima yako na kukushauri au kukubadilisha kwa heshima na Upendo, hata uwe jambazi utarudi kawaida.

Anaweza akawa hajui kutafuta pesa, ila akakupikia vizuri, akakusaidia kusimamia watoto na nyumba, hii ni kukufanya uwe successful kwani asingekuwepo ungeumiza kichwa nani afue, apange nyumba n.k

Mwanamke mwenye akili anajua anaweza kuchat upuuzi na wanaume Nje, anajua anaweza kuvua chupi Yake alale Nje ila MILELE HAWEZI VUNJA NYUMBA YAKE MWENYEWE.

Behind every failure man, there is a bitch.
Kama mwanaume havuti bangi wala madawa, na alikua na mafanikio, ukiona kafulia, kaanguka kuna a bitch, a bitch anaweza akawa  mchepuko wake aliyotaka kuufanya mke  au mke wake aliyemvunjia heshima au vyote.

Na katika yote Mungu zaidi ya yote huweza kukurejesha kwenye status yako


Sunday, August 6, 2017

CHEZEA VYOTE SIO MOYO

Asilimia kubwa ya wanaume wanapoenda kumuaproach mwanamke hua wapo seriosly na wanachoitaji,lkn wachache wao hawapo ivyo


hua wanaenda kumtaka mwanamke kwa kumpima imani tuu au kujaribu jee ana moyo wa aina gani??kipindi ambacho wewe unaenda kumuaproach akilini mwako unasema yule hakosi mtu


kumbe pengine kipindi unatuma maombi yako maskini bidada wa watu yupo single,unapoamua kumwambia nakupenda,unakua unasema tuu lkn moyoni mwako ushajipa point kama huyu ni demu wa mtu tuu so akikubali its ok akikataa fresh tuu


kumbe unakuta yule bint alikua single kwa kipindi flani na sasa anaamua rasmi kusema im ready ntaingia tena kwenye mahusiano kwa ataeniaproach nikavutiwa nae,ndoano ulorusha inatiki kibahati nzuri unapata jibu zuri kwamba sawa nimekubali kua nawe,wakati anajibu mwenzio alimaanisha kutoka moyoni lkn kumbe wewe upo kwenye pata potea,,end of the day anakukabidhi moyo akidhani amepata mtu tayari kumbe maskini ulikua kwenye majaribu


inauma akigundua aliempa moyo alikua na nia ya kuuchezea,maumivu ya mapenz kwa watoto wa kike asilimia 70 hua yanasababisha madhara,ukitahamaki unaweza kumsababishia hata maradhi ya moyo bila ya wewe mwenyewe kujua coz alishajipa mia kwa mia anakuja kukuta kumbe aliingia choo cha kiume sasa akojoe wima?


more than pain,,wanaume kueni makini unapoamua kumfata mtu kumueleza hisia zako uwe unamaanisha kutoka moyoni,,yule unaemchezea moyo wake nae kiumbe na anajua kabisa hapa nimeshabugi unafkiri nini kinachofata kama sio kukuepuka?akikuepuka unamuangushia lawama yeye ili hali wewe ulieanza huoni kosa lako?


akiamua kuamisha hisia akamkabidhi mwingine unajikuta unaumia why??cheza na vyote lkn sio moyo wa mtu,unapomfata mtu kumueleza hisia zako hakikisha UNAMAANISHA,,,


Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...