Thursday, February 20, 2020

Kfc kuku

UPISHI WA KUKU WA KFC,,,,
MAHITAJI
KUKU
UNGA WA NGANO(UNGA UTIE CHUMVI KIDOGO, PILIPILI YA UNGA, PILIPILI MTAMA YA UNGA, BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA)
MAFUTA YA KUPIKIA
KITUNGUU SWAUM
TANGAWIZI MBICHI
MAYAI
CHUMVI
NDIMU

MATAYARISHO
1,,,,,OSHA KUKU WAKO,,, PONDA KITUNGUU SWAUM NA TANGAWIZI MTIE KUKU WAKO, TIA NA CHUMVI NA NDIMU,HALAFU MFUNIKE KAMA DK 20 ILI VIUNGO VIKOLEE,, UNAWEZA PIA KUTIA BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA...

2,,,,CHUKUA SAHANI WEKA UNGA WAKO WA  NGANO,,,, CHUKUA BAKULI PASUA MAYAI YATIE CHUMVI KIDOGO(WINGI WA MAYAI INATEGEMEA NA KIASI CHA KUKU)

3,,,,CHUKUA KIPANDE CHA KUKU KICHOVYE KWENYE MAYAI,,,, HALAFU KICHOVYE KWENYE UNGA,,,, KIRUDIE TENA KUCHOVYA KWENYE MAYAI KITIMBUKIZE JIKONI KWENYE KALAI LA MAFUTA,,,, KAANGA MPAKA KUKU AKIWA BROWN TAYARI KWA KULIWA


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...