Tuesday, March 10, 2020

Fish balls

FISH BALLS

MAHITAJI

Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi)
Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa
Carrot ndogo 1 (iloparwa kama chipsi)
Chumvi ya kiasi
Pilipili ya kuwasha 1 kubwa (paste)
Ndimu ya kiasi
Breadcrumbs 1/2 cup
Pilipili manga 1/2 tsp (powder)
Coriander (majani ya giligilani) 2 tbsp

JINSI YA KUTENGENEZA

Watoe tuna maji yote wawe wakavu waeke kwenye bakuli changanya na vitu vyote ila breadcrumbs weka kjk na nusu, ilobaki utatumia baadae

Changanya vizuri than fanya viduara kama hivo pakaa  breadcrumbs panga kwenye trey ya kuchomea choma kwenye oven moto 170 kwa dakika 20 watoe tayari kwa kuliwa


Lemon curd

LEMON CURD FOR CHEESE CAKE

MAHITAJI
Corn starch 3 tblsp
Maji kikombe 1
Malimau 2 (yakamue)
Sukari 1/2 kikombe
Kiini cha yai (egg yolk) 1
Rangi ya keki ya njano kidogo sana

MATAYARISHO
Baada ya cheese cake kuwa kwenye friji kama masaa 4 ndio anza kufanya hii process. Itoe cake kwenye friji. Iweke pembeni.

Changanya corn starch, maji, juice ya limau na sukari weka kwenye sufuria halafu weka kwenye jiko koroga mpaka yashikane.

Yakisha kuwa nzito  wacha kwa moto mdogo mdogo.

Kwenye kibakuli piga kiini cha yai mpaka kichanganyike vizuri. Chukuwa ule uji ulioko kwenye jiko kama vijiko viwili vikubwa changanya na kiini piga haraka haraka ili yasitokee madonge.
Halafu mimina kwenye ule uji koroga vizuri halafu tia rangi ya njano. Uzito wake uwe kama hivyo kwenye picha. Ukiona nyepesi ongeza corn starch na ukiona nzito ongeza maji.

Acha kwa dakika kama mbili halafu zima moto weka pembeni ipowe kidogo

Mimina kwenye cake halafu weka kwenye friji kwa masaa kama 3 Itakuwa tayari kwa kuliwa

Unaweza, kutumia kwenye keki yeyote sio lazima cheese cake

Pia unaweza kutumia kwenye vileja


Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...