LEMON CURD FOR CHEESE CAKE
MAHITAJI
Corn starch 3 tblsp
Maji kikombe 1
Malimau 2 (yakamue)
Sukari 1/2 kikombe
Kiini cha yai (egg yolk) 1
Rangi ya keki ya njano kidogo sana
MATAYARISHO
Baada ya cheese cake kuwa kwenye friji kama masaa 4 ndio anza kufanya hii process. Itoe cake kwenye friji. Iweke pembeni.
Changanya corn starch, maji, juice ya limau na sukari weka kwenye sufuria halafu weka kwenye jiko koroga mpaka yashikane.
Yakisha kuwa nzito wacha kwa moto mdogo mdogo.
Kwenye kibakuli piga kiini cha yai mpaka kichanganyike vizuri. Chukuwa ule uji ulioko kwenye jiko kama vijiko viwili vikubwa changanya na kiini piga haraka haraka ili yasitokee madonge.
Halafu mimina kwenye ule uji koroga vizuri halafu tia rangi ya njano. Uzito wake uwe kama hivyo kwenye picha. Ukiona nyepesi ongeza corn starch na ukiona nzito ongeza maji.
Acha kwa dakika kama mbili halafu zima moto weka pembeni ipowe kidogo
Mimina kwenye cake halafu weka kwenye friji kwa masaa kama 3 Itakuwa tayari kwa kuliwa
Unaweza, kutumia kwenye keki yeyote sio lazima cheese cake
Pia unaweza kutumia kwenye vileja
Tuesday, March 10, 2020
Lemon curd
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Fish balls
FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...
-
#biriani #goatbiriani #beefbiriani #birianiyambuzi Mahitaji 1.Mchele wa Basmat 1/2 Kg 2.Nyama ya Mbuzi Stake 1/2 Kg 3.Viazi mbatata viku...
-
Jinsi ya kutengeneza lipbam Aina ya kwanza mahitaji Vaseline /mafuta yoyote ya mgando yani petroleum jelly Mafuta ya Nazi Asali Rangi ...
-
MAKARONI mahitaji makaroni pacti (1) tomato fresh (4-5) kitunguu maji (1-2) hoho (1) karoti (1) maji ya moto kiasi nyama nusu ma...
No comments:
Post a Comment