Tuesday, July 11, 2017

FAIDA 5 ZINAZOPATIKANA KWENYE MAJI YA NDIMU



Faida 5 za Kunywa Maji Yenye Ndimu

Faida 1. Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

Faida 2. Huboresha Kinga za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

 
Faida 3.Husaidia Unyonywaji wa Madini Mwilini

Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

Faida 4. Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicalsmwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

 Faida 5.Husaidia Kupunguza Hatari ya Kiharusi

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...