Tuesday, July 11, 2017

AINA SABA YA MATUNDA YANAYOSAIDIA KUKATA MAFUTA TUMBONI

KUPUNGUZA MLUNDIKANO WA MAFUTA TUMBONI


Tuangalie kwa umakini sana njia saba ambazo huondoa haraka mafuta tumboni kwa kutumia matunda,
Zipo aina nyingi sana za vyakula/matunda ambavyo hutumika ktk kupunguza tatizo la mafuta tumboni,lkn leo nawaletea aina hizi saba za matunda ambayo tunatumia kila siku majumbani mwetu lkn hatujui kwa kiasi gani ni vizuri zaidi ktk kuondoa tatizo la mafuta mengi tumboni yanayopelekea mtu kua na kitambi iwe ni kwa wanawake au wanaume




1,,NYANYA

Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.

2,, TANGAWIZI

Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.





3,,JUISI YA LIMAU

Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.



4,,TIKITI MAJI

Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.



5,,TANGO

Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.

6,,PARACHICHI

Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba). Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.

Kula parachichi 1 kila siku.

7,,TUFAA

Kula tufaa maarufu sana kama 'apple' (epo) kunaweza kusaidia kupigana na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa mengi sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.

Hivyo kula tunda hili 1 kila siku asubuhi kupunguza shauku yako ya kutaka kula zaidi ndani ya hiyo siku


1 comment:

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...