Wednesday, July 12, 2017

ZINGATIA VITU VITATU ILI UDUMU NA MWENZA WAKO

Inawezekana alishakutana na wengi wazuri,wenye sifa,muonekano na uwezo wa kila kitu lkn hakudumu nao,

Hii sio kwamba hawakumpendeza,sio kwamba hakuwapenda,sio kwamba hakupanga malengo yakuishi nao,ila tuu ni kutokana na wao hawakujua kutunza vitu muhimu vitatu

Unapoamua kuanzisha nae mahusiano unatakiwa ujiwekee ndoto kwenye akili yako ya kwamba huyu ndie chaguo langu na ndie ntazeeka nae

Lkn kama ukiingia kwa mguu mmoja ndani mmoja nje hautajiwekea hiyo ndoto akilini kamwe,utakua mtu wa kusua sua tuu bila mpangilio maalum huku ukishuhudia watu wakimaliza miaka kwenye ndoa zao,


Kanuni kuu ya kudumu nae ni kusema na hivi vitatu kwanza
1...moyo
2...mdomo
3...macho

Hivi vitu vitatu ni vitu vya kuviogopa sana,kwa sababu ndio vitu vikuu vinavyotuponza kila siku kwenye maisha yetu,

Chunga sana moyo wako usije ukabadili msimamo wako kwa umpendae ukajikuta moyo unaangukia kwingine kumbe ni tamaa tuu kule wala hupendwi unakwenda kupoteza muda wako tuu kwa kudanganywa huku ukimuacha yule muhimu ambae alikupenda kwa dhati,,

Chunga sana mdomo wako,mdomo ndio unaoongoza kuponza wengi kwenye mahusiano/ndoa,kabla hujaongea anza kufikiri kichwani kwanza je!hiki nnachotaka kuongea kitampendeza mwenzangu?ukiona kina hitilafu ni bora kuacha,maana siku zote kuna msemo usemao ni bora kukaa kimya kuliko kuongea mpaka unyamazishwe,,mahusiano yaliyo bora hayaitaji mdomo kuongea sana yanahitaji matendo tuu yakuonesha ni jinsi gani unakubali juu ya uwepo wake kwako,,,


Chunga sana macho yako,na hasa mnapokua sehemu za watu,acha kukodolea macho visivyokuhusu mbele yake hiyo ni mbaya na inaweza kukushusha haraka bila mwenyewe kujijua,,,


Maarifa yako yamo ndani ya akili yako,,jichunguze je!upo makini ktk ivyo vitu vitatu???

Jikosoe na ujibadilishe utaamini nnalosema na mtadumu miaka yote


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...