Wakati mwingine hua tunajichosha kwa kujipa msongo wa mawazo kwa jambo la kujitakia
Unaweza ukaishi nae kwa salama na amani tuu hata miaka 20,lkn likaja kutokea lakutokea likasababisha mfarakano baina yenu
Hakuna hitimisho sahihi lililopo mbele yenu zaidi ya kuachana,je!utafosi uendelee nae kwa kisingizio kua tumetoka mbali?
Ndipo niliposema kujitafutia misongo ya mawazo isiyo na msingi,
Najua inauma na hasa kwa mliopendana kidhati lkn ikumbukwe kua kuna neno lisemwalo kua hakuna marefu yasiyo na ncha,,,au kila lenye mwanzo halikosi mwisho
Ukikubaliana na haya utaamini ni kweli nisemacho ingawaje moyoni kinauma tena maumivu yake hayasemeki
Jaribu kuukubali ukweli kua yameshatokea
Jaribu kuupa moyo nafasi nyingine huenda ni bora pia kuliko ulipotokea
Kila likuepukalo lina heri ndani yake
Kuforce sana vitu visivyowezekana kunaweza kufupisha maisha yako
Sisemi umuache kirahisi,jaribu kupambana ili uwe nae,lkn kama ikishindikana jifunze kuukubali ukweli kua haiwezekani na upige moyo konde kuanza kupiga hatua mpya itayokusogeza mahali pengine
#Achaibakistory
No comments:
Post a Comment