Sunday, July 16, 2017

UTANI HUZIDISHA UPENDO

UTANI HUIMARISHA UPENDO
Jizoesheni kutaniana pindi mnapokua faragha,utani una nafasi kubwa sana kwenye kuzidisha upendo lkn usizidi mipaka ikapelekea ule utani kusababisha mmoja wenu akachukia

Si vizuri kuishi ndani kama mazimwi,na hii ni asilimia kubwa kwa wanaume pirika za utaftaji hupelekea kua seriosly sana hata akiwa na mwenza wake chumbani

Hujikuta muda wote kakunja sura hali inayopelekea hata mke kuogopa kuanza kumtania,jaribu kukunjua paji lako la uso pindi tuu uanzapo kuona kibaraza cha nyumba yako

Usimkunjie uso sana mwenza wako kiasi kwamba mida ikikaribia kurudi nyumbani anaanza kuingia unyonge kwa kufikiria unavomkunjiaga sura kila siku

Na kwa upande wa wanawake pia jitahidi sana kumchokoza mwenza wako kwa viutani vidogo vidogo ata kama alikua na uchovu wa kazi za kutwa nzima ajiskie nafuu kutokana na jokes za hapa na pale

Kingine pia mwanamke anaweza kua chanzo cha mume kua na hali hiyo ya kisrani kila arudipo nyumbani kutokana na visa na kero unazomfanyia

Jaribu kua mcheshi kwa mwenzio kiasi kwamba ata akiwa kazini awe anaona kama saa haziendi ili awahi kurudi nyumbani mapema kutokana unakua unamfanya ajiskie vizuri kwa vijokes vyako vya hapa na pale

Mwanamke jiweke msafi muda ote na hasa manukato mazuri yazidi kipindi ambacho unajua mida hii mume anarejea nyumbani,ili ile hali yakumfanya akuchukie kwa kiharufu kibaya isiwepo


Hiyo points ya usafi ni mojawapo ya sababu nyingi kwa wanaume kua na visrani nyumbani mana hana raha,anaingia unyonge mida ya kurudi ikifika ikiwa tuu anawaza hali atayoikuta uko nayo


Nitaizungumzia zaidi kwenye kipengele kingine cha usafi kwa wote wawili kwa wakati mwingine lkn leo hii tuangazie hapo kwenye mada husika ya kutaniana


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...