Monday, July 31, 2017

WAKATI NI UKUTA

Kuna baadhi yetu hua tunajisahau sana kwa kuhisi labda apa tulipo ndo tumeshafaulu maisha,hatukai tukajiuliza kwamba kuna kesho tunahitaji kujenga familia kama walivoishi wazazi wetu,

Ni misingi mizuri ikiwa utakaa japo dk kumi ukajitafakari ulikua wapi?upo wapi?na unaelekea wapi??ukipata muda wakutafakari hilo utaelewa maana yangu,,,,,

WAKATI NI UKUTA usije kustuka muda ushapotea unaishia kuangalia maisha ya wenzio na familia zao,,,,,,

Ndipo unaanza kutamani kua na familia ukiangalia umri umeshakutupa,maisha umeshayachezea,kila kitu kipo tofauti na matarajio

Amsha akili yako kwa kuonea wivu wenzio,kwanini wao waweze wewe ushindwe?utakua ni ulimbukeni wa akili kwa kusindikiza wenzio kila siku

Hata vitabu vya dini viliandika muda ukifika unatakiwa ujenge familia kwa kuoa/kuolewa

Starehe zina mwisho wake,ujana una kikomo chake,lkn pia ukumbuke umri nao una mwisho wake,,jaribu kutafakari,,,,,,,


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...