Wednesday, November 15, 2017

UPISHI WA BIRIANI

#biriani #goatbiriani #beefbiriani #birianiyambuzi
Mahitaji
1.Mchele wa Basmat 1/2 Kg
2.Nyama ya Mbuzi Stake 1/2 Kg
3.Viazi mbatata vikubwa 1/4Kg
4.Vitunguu maji 1/2 Kg
5.Nyanya Kubwa 4
6.Nyanya ya Paket 1
7.Biriani Masala 1/2 Kijiko cha chakula
8.Viungo vya pilau 1/2 Kijiko
9.Sukari 1/2 Kijiko
10.Chumvi kiasi
11.Mtindi 1/2 Kikombe
12.Vinegar au Ndimu
13.Kitunguu thomu kilotwangwa Kijiko cha chai
14.Tangawizi iliotwangwa kijiko cha chai
15.Karot ilioparwa 1
16.Pilipili hoho iliokatwa 1
17.Mafuta ya kupikia 1/2 Lita
18.Rangi nyekundu
19.Maji Kiasi
20.Curry Powder

Maandalizi
1.Osha mchele na uroweke kwa robo saa
2.Kata kata nyama osha weka tangawizi, chumvi, curry powder na kitunguu thomu
3.Menya vitunguu osha na katakata weka pembeni
4.Menya viazi osha weka rangi vipete vizuri
5.Saga nyanya au zipare

Jinsi ya kupika
Rosti la Biriani
1.Weka nyama acha ikauke kidogo kisha weka maji taratibu mpaka iive iwe laini sana
2.Weka mafuta kwenye karai yakipata moto vizuri weka vitunguu maji vikaange mpaka viwe na rangi ya dhahabu
3.Toa vitunguu weka viazi mbatata kisha vikaange kidogo na uvitoe
4.Weka sufuria na mafuta kidogo uliokaangia vitunguu
5.Yakipata moto mimina karoti kaanga kidogo
6.Weka pilipili hoho kaanga kidogo
7.Malizia kuweka kitunguu thomu
8.Kisha mimina nyanya, chumvi kidogo na viazi acha vichemke kama dakika 3
9.Mimina nyama na supu yake acha kwa dakika kadhaa
10.Weka nyanya ya Paket, vinegar na mtindi acha vichemke
11.Weka viungo vya pilau, biriani Masala na sukari koroga acha ichemke kidogo
12.Malizia kuweka vitunguu ulivyo vikaanga
13.Acha dakika 3 epua rosti lako acha lipoe

Wali wa Biriani
1.Weka maji kwenye sufuria na chumvi
2.Yakichemka weka mchele wako mpaka uive
3.Nyunyizia mafuta na rangi nyekundu kwenye wali wako ufunike acha ukauke

Kupakua
1.Changanya wali vizuri ili rangi ichanganyike na wali vizuri
2.Chukua rosti la biriani vijiko vitano weka kwenye wali wako changanya vizuri
3.Pakua wali kwenye sahani
4.Koroga rosti vizuri pakua na weka katikati ya sahani
5.Tayari kwa kula.


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...