Thursday, November 2, 2017

UPISHI WA KATRESS

YOYO CUTLETS / YOYO KATLESI  :

Mahitaji :

Mayai yalochemshwa – 4
Biskuti – 5 zilovunjwa na kuwa unga
Viazi mviringo – 250 gms, chemsha, toa maganda, viponde
Kitunguu maji – 1, kilichokatwa katwa
Yai– 1, lilopigwa
Pilipili ya unga – kjk 1 cha chai
Kotmiri– kiganja 1 yalokatwa katwa
Chumvi kiasi
Mafuta

Maelekezo :
1. Chemsha mayai yakisha iva weka pembeni... Chemsha viazi vikishaiva..  menya na weka  kwenye bakuli viazi, vitunguu, pilipili ya unga, chumvi na kotmiri
2. Changanya vizuri
3. Weka mayai yalochemshwa na fanya madonge ya kiasi na kandamiza kidogo
4. Piga yai katika bakuli...Chovya katlesi kwenye yai lilopigwa kisha garagaza kwenye unga wa biskuti
5. Weka mafuta kwenye kikaango yapate moto
6. Kaanga katlesi mpaka ziwe na rangi ya dhahabu
7. Pambia kwa kotmiri
8. Andaa kwa kuliwa


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...