Doughnut/donut
MAHITAJI
1.Unga – ROBO kilo
2.Sukari-100 grams
3.Mayai 5
4.blueband/Siagi - 4 Vijiko vya chakula
5.Hamira 1 Kijiko cha chakula
6.Baking Powder - 1 Kijiko cha chai
7.Vanilla - 1 Kijiko cha chai
8.Hiliki zilizosagwa - 1 Kijiko cha chai
9.icing sugar– robo kilo
MATAYARISHO
1.Unavunja mayai,unatia sukari,hamira, baking powder,vanilla na hiliki ikisha unakoroga kwa kutumia kikorogeo cha kukorogea keki.Unakoroga mchanganyiko kwa muda wa dakika 5.
2.Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe ya moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unakoroga tena kwa dakika mbili tu.
3.Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa kisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono,mpaka ulainike.
4.Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa,na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.
5.Sukuma na ukate madonge.Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakati ya madonge.
6.Ukimaliza kukata madonge yote,yaweke kidogo yavimbe halafu weka mafuta na uyakaange.
7.Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe yamoto moto kisha yachovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu.
8.Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Thursday, February 20, 2020
Donught
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Fish balls
FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...
-
#biriani #goatbiriani #beefbiriani #birianiyambuzi Mahitaji 1.Mchele wa Basmat 1/2 Kg 2.Nyama ya Mbuzi Stake 1/2 Kg 3.Viazi mbatata viku...
-
Jinsi ya kutengeneza lipbam Aina ya kwanza mahitaji Vaseline /mafuta yoyote ya mgando yani petroleum jelly Mafuta ya Nazi Asali Rangi ...
-
MAKARONI mahitaji makaroni pacti (1) tomato fresh (4-5) kitunguu maji (1-2) hoho (1) karoti (1) maji ya moto kiasi nyama nusu ma...
No comments:
Post a Comment