Thursday, February 20, 2020

Mandaz

Maandazi
Mahitaji
1,,,,,, unga kilo moja
2,,,,,,nazi moja tui lijae kikombe
3,,,,sukari nusu kikombe utachopimia tui
4,,,,,,,chumvi robo kijiko kidogo
5,,,,,,,,amira kijiko chakulia chakula kimoja na robo
6,,,,,,,baking poda sio lazima ila ukitaka unaeka robo kijiko kidogo kiasi sawa kama chumvi
7,,,,,,mafuta unayokandia vijiko 6 vya kulia chakula
8,,,,,iriki ilosagwa kijiko kidogo au punjepunje upendavyo mwenyewe,,,
    Ukishachanganya vyote Anza kukanda unga wako ukiwa unaganda mikononi  pakaza unga mikono yako kidogo kidogo uku unaendelea kukanda mpaka uhakikishe unga haunasi mkononi,,, acha unga ukae dk 5 tu alafu Anza kukata maandazi yako, ukishakata yaache kiasi kama cha robo saa au dk 20 inategemea na Hali ya hewa, kama baridi yataitaji muda wa ziada, muhimu tuu yasiumuke Sana yatapasuka jikoni, alafu utaanza kuchoma uku unaligeuzageuza andazi pande zote mbili, unapokata andazi usiliache na nyama nyingi alitoiva ndani, sukuma unga kiasi karibia kama chapati lkn pia usisukume Sana likawa jepesi zaidi litakua kaukau, kua makini kwenye kusukuma ukisie tuu kiasi chakusema lishatosha utaanza kukata


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...