Thursday, February 20, 2020

Halfkeki

HALF CAKE

MAHITAJI
Unga wa ngano  Nusu
Sukari robo
Baking powder nusu kijiko, kile kidogo
Magadi soda (bicarbonate soda)  kijiko cha chai 1,kile kidogo
Mafuta 2 vijiko vya chakula
Mafuta ya kukaangia
Maji ya uvuguvugu kiasi

MATAYARISHO

Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea)kisha ukande(hakikisha unakuwa mgumu)

Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi)

Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke.

Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani.

Zikisha iva zitoe na uiweke kwenye chujio ili zichuje mafuta.

Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...