Thursday, February 20, 2020

Vish

.Visheti vya kokoto
MAHITAJI
siagi robo
Sukari robo
Maziwa ya unga vijiko 2 vya chakula
Baking powder kjk 1cha chakula
Unga wa ngano nusu
Yai 1
Vanilla au ladha yoyote kijiko 1
Mafuta ya kupikia nusu lita

MATAYARISHO

Saga sukari na siagi pamoja mpaka ilainike weka yai.
mix vizuri halafu weka unga, vanila kijiko kimoja, baking powder na unga wa maziwa changanya vizuri.
weka maji kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wako mpaka uwe donge moja USIJAZE maji  na wala usiwe mgumu sana.

Ugawe madonge  8
chukua kila donge sokota kama kamba na ukate vipande vidogo vidogo dizain ya kokoto,,

weka mafuta  jikoni yakipata moto weka visheti vyako  mpaka viive visiwe vyekundu sana.
toa viweke pembeni vipoe.

MATAYARISHO ya shira
👇👇
Weka sufuria  kwenye jiko weka maji kikombe kimoja na sukari kikombe kimoja, acha ichemke mpaka iwe nzito

utaona inaaza kuganda pembeni mwa sufuria
weka vanilla na visheti punguza moto uwe mdogo
Mix mpaka viwe vikavu kabisa (vizuri kuvi mix kwa kuliinuwa sufuria  na kuvipeta ili visivurugike). Tayari kwa kuliwa


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...