Upishi wa vitumbua
MAHITAJI
UNGA wa mchele nusu(roweka mchele usiku, mpaka asubuhi usage kwenye Brenda, au PELEKA mashine)
Sukari nusu kikombe
Yai moja
Iriki kijiko kidogo
Amira kijiko 1 cha chakula
Mafuta ya kupikia
Unga wa ngano kijiko kimoja
Tui bubu kikombe kimoja
MATAYARISHO
AWAMU YA KWANZA:
Kama unatumia mchele ulioroweka umwage maji utie kwenye Brenda na vitu vyote (kasoro mafuta,) ,,
usage mpaka UHAKIKISHE vimelainika kabisa
Mimina kwenye bakuli UFUNIKE uache uumuke
Ukishaumuka andaa chuma chako cha vitumbua, kiweke jikoni tia mafuta vishimo vyote,,, hakikisha mafuta yamepata moto Anza kuchoma vitumbua vyako,,, baada ya dakika chache pindua juu kuwe chini ili kiwive pande zote
Ukiona kimekua brown tayari unaweza kutoa ili usiunguze kua makini na moto kulingana na jiko unalopikia
AWAMU YA PILI:
kama unatumia unga ulosaga mashine, utie kwenye bakuli na vitu vyote koroga vichanganyike, UFUNIKE mpaka uumuke ndo uanze kuchoma vitumbua vyako
ANGALIZO,,,, kulingana na mchele husika unaotumia ukiona uji wako mzito zaidi, ongeza VIMAJI kidogo maana uji ukiwa mzito Sana vitumbua haviwivi ndani
Thursday, February 20, 2020
Vitumbua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Fish balls
FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...
-
#biriani #goatbiriani #beefbiriani #birianiyambuzi Mahitaji 1.Mchele wa Basmat 1/2 Kg 2.Nyama ya Mbuzi Stake 1/2 Kg 3.Viazi mbatata viku...
-
Jinsi ya kutengeneza lipbam Aina ya kwanza mahitaji Vaseline /mafuta yoyote ya mgando yani petroleum jelly Mafuta ya Nazi Asali Rangi ...
-
MAKARONI mahitaji makaroni pacti (1) tomato fresh (4-5) kitunguu maji (1-2) hoho (1) karoti (1) maji ya moto kiasi nyama nusu ma...
No comments:
Post a Comment