Friday, July 21, 2017

JIFUNZE KUIMARISHA FURAHA YAKO

Inakuaga ni siku ya furaha sana na hujihisi ni pekee mwenye bahati kwenye dunia kwa mungu kukuunganisha nae,

lkn cha ajabu furaha hutawala kipindi kifupi sana kwa wengi wetu,

ni wachache sana wanaodumu na hii furaha kwenye ndoa zao

Haimaanishi labda hukujipanga kua nae,umeshinikizwa?jibu linabaki hapana,kwanini hapana?ulifanya maamuzi sahihi kwa kujua sasa nina mtu sahihi

Jambo lakujiuliza ni kwa nini sasa hii furaha isiendelee?nini kikwazo?ikiwa mlikubaliana na mkawa na lengo moja lakuungana kua mwili mmoja?


Asilimia kubwa mie husema ni ushetani tuu unaopita kati yenu,siku zote adui wa ndoa zote ni shetani,kwanini mumpe nafasi shetani?ikiwa mnamjua vizuri hapendi kuona watu wakiwa pamoja na furaha zao kwenye ndoa

Muepuke na kama hujui njia za kumuepuka fuata haya yafuatayo


Kwanza kabisa mtangulize Mungu kwa kila kitu,,pili jaribu kua karibu na wazazi pande zote mbili ili hata zikianza dosari wazee wawe na nguvu yakusolve coz wao ndio ngao yako siku zote


Tatu,epuka marafiki wanafki na hasa upande wa mwanamke,,hii ipo pande zote ata upande wa mwanaume pia anao marafiki wanafki lkn kuna unafuu wa kustahmili mikiki kwa mwanaume tofauti na wanawake mioyo yao miepesi


Jiwekee kiapo cha nafsi kwamba ndo huyu huyu simuachi hata iweje,nimeshamvaa na siwezi kumvua kamwe kwenye shida ntakufa nae na kwenye ntakula nae


Maongezi mazuri mdomoni na tabasamu la usoni siku zote za maisha yako


Upole,unyenyekevu,kujali,hisia zake ziwe zako muda wote awepo au asiwepo,,kila gumu analopitia mnasolve pamoja kwa kupeana moyo


Huruma pindi mmojawapo amekwama,sio kipindi cha raha unafurahika akikwama tuu unambadilikia hiyo haitakujenga kamwe


Jitahidi sana kubuni mbinu mpya kila siku ili asikuone yule yule tuu,,ajaribu kukuona mpya kila siku za maisha yake



Pendeleeni kutoka pamoja nyakati za jioni,tembeleeni ndugu na jamaa,wazazi na hata wagonjwa mahospitalini ili mpate baraka zao

Yapo mengi ili kuidumisha furaha yako ndani ya ndoa yako lkn kwa leo naishia hapo tukutane wakati ujao


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...