Friday, July 28, 2017

OGOPA SANA CHOZI LA MWANAMKE

Hili linajulikana wazi halina ubishi,asilimia kubwa sana ya wanaoongoza kwa uvumilivu kwenye mahusiano/ndoa ni wanawake

Hii ni kutokana na mioyo ya uvumilivu waliopewa na mungu,,

Simaanishi kwamba wanaume hawana uvumilivu laa,,,,wanao uvumilivu tena  sana lkn asilimia zao zipo chini tofauti na mwanamke


Mwanamke ana uwezo wa kudumu na mume mlevi ata miaka 50,ana uwezo wakukufumania ata mara mia na bado akakusamehe,

Anaweza kuishi na mwanaume mpigaji yeye kila siku mwili wake ni kama ngoma lkn bado akakusamehe

Utadumu nae miaka mingi kutokana na uvumilivu wake lkn tambua ya kwamba machozi yake ni sumu kubwa kwenye maisha yako

Jaribuni kua waelewa wanaume,na hasa nyakati izi tulizonazo za utandawazi,,usijaribu kuuchezea sana moyo wa mwanamke hiyo ni laana


Atakuvumilia sana,atateseka sana na hiyo yote ni kwa sababu ya mapenzi yake ya dhati alonayo kwako

Lkn siku atakayoamua kusema basi,ile basi yakutoka moyoni basi ujue ndio basi

Ngumu kuurudisha moyo wake nyuma sana sana anaweza ata kukuwekea sumu kwenye chakula ambacho mtakula pamoja ili mfe wote

OGOPA SANA CHOZI LA MWANAMKE


No comments:

Post a Comment

Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...