MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA .
Vipimo
Unga 1 ½ vikombe vya chai
Mafuta ¼ kikombe cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Maji 1 kikombe cha chai
Mafuta ½ kikombe cha chai
Mayai 6 mayai
Manda nyembamba za mraba
(Spring roll pastries sheet) 6
Nyama ya kusaga ½ kilo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 1 kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwakatwa ½ kikombe
Chumvi kiasi
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Pilipili mbichi kiasi (ukipenda)
Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike
Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1.
Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe.
Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba .
Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha.
Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi.
Weka kwenye sahani tayari kuliwa
Tuesday, July 11, 2017
UPISHI WA CHAPATI ZA NYAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Fish balls
FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...
-
MKATE WA MCHELE/MKATE WA KUMIMINA Mahitaji 1.Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai) 2.Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai) 3...
-
Naomba nikujuze mambo matano muhimu yakuimarisha afya yako ila kumbuka awali ya yote mazoezi ni muhimu kwa afya yako. 1. unaishi sehemu yen...
-
Huu ni mchanganyiko ambao unakupa nguvu na afya,kuna vitu vitano ambavyo vyote ni muhimu kwa afya yako humo 1,,ndizi 2;;parachichi 3;;app...
No comments:
Post a Comment