Tuesday, March 10, 2020

Fish balls

FISH BALLS

MAHITAJI

Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi)
Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa
Carrot ndogo 1 (iloparwa kama chipsi)
Chumvi ya kiasi
Pilipili ya kuwasha 1 kubwa (paste)
Ndimu ya kiasi
Breadcrumbs 1/2 cup
Pilipili manga 1/2 tsp (powder)
Coriander (majani ya giligilani) 2 tbsp

JINSI YA KUTENGENEZA

Watoe tuna maji yote wawe wakavu waeke kwenye bakuli changanya na vitu vyote ila breadcrumbs weka kjk na nusu, ilobaki utatumia baadae

Changanya vizuri than fanya viduara kama hivo pakaa  breadcrumbs panga kwenye trey ya kuchomea choma kwenye oven moto 170 kwa dakika 20 watoe tayari kwa kuliwa


Lemon curd

LEMON CURD FOR CHEESE CAKE

MAHITAJI
Corn starch 3 tblsp
Maji kikombe 1
Malimau 2 (yakamue)
Sukari 1/2 kikombe
Kiini cha yai (egg yolk) 1
Rangi ya keki ya njano kidogo sana

MATAYARISHO
Baada ya cheese cake kuwa kwenye friji kama masaa 4 ndio anza kufanya hii process. Itoe cake kwenye friji. Iweke pembeni.

Changanya corn starch, maji, juice ya limau na sukari weka kwenye sufuria halafu weka kwenye jiko koroga mpaka yashikane.

Yakisha kuwa nzito  wacha kwa moto mdogo mdogo.

Kwenye kibakuli piga kiini cha yai mpaka kichanganyike vizuri. Chukuwa ule uji ulioko kwenye jiko kama vijiko viwili vikubwa changanya na kiini piga haraka haraka ili yasitokee madonge.
Halafu mimina kwenye ule uji koroga vizuri halafu tia rangi ya njano. Uzito wake uwe kama hivyo kwenye picha. Ukiona nyepesi ongeza corn starch na ukiona nzito ongeza maji.

Acha kwa dakika kama mbili halafu zima moto weka pembeni ipowe kidogo

Mimina kwenye cake halafu weka kwenye friji kwa masaa kama 3 Itakuwa tayari kwa kuliwa

Unaweza, kutumia kwenye keki yeyote sio lazima cheese cake

Pia unaweza kutumia kwenye vileja


Thursday, February 20, 2020

Sponge cake part 3

Tutakua tushapata michanganyiko miwili,,,, Hapa Sasa michanganyiko yote miwili imeshakutana kwenye bakuli moja


Tunamimina Sasa kwenye chombo  chetu cha  kupikia, ili tuweke kwenye moto(jikoni)

MOTO 180,dk 35


Part 2 sponge cake

Hatua ya pili Chukua bakuli lenye viini Anza kutia maziwa uku unakoroga endelea kutia mafuta ya kula, pamoja na vanilla koroga mpaka vichanganyike halafu chota unga wa mkono uwe unatia kidogo kidogo uku ukiendelea kuchanganya mpaka vichanganyike vyote,,, tafadhali huu mchanganyiko wa pili USITUMIE mashine yoyote, tumia mixer ya mkono(whisk) au mwiko tu,ukimaliza hapo changanya michanganyiko yako yote sehemu moja,, yaan unachota huo mchanganyiko wa  ute ulosaga kwa kutumia  kijiko unatia kwenye bakuli lenye viini mix vizuri mpaka mchanganyiko wako uwe  sawa


Keksponge

Part1, keki laini ya sponge,,,

Tuangalie Mahitaji kwenye hii keki yetu:

Unga wa ngano gram 150 ambayo ni Sawa na vijiko 10 vya kulia chakula,,,sukari gram 60 ambayo ni Sawa na vijiko vinne mpaka vitano vya kulia chakula,,, mayai manne, maziwa ya maji vijiko 7 mpaka 8, ambayo ni MLS 90 mpaka 100 sio mbaya,,mafuta ya kupikia vijiko 8 ambayo ni MLS 60,,baking powder kijiko kimoja kidogo cha kukorogea chai,, ladha ya vanila kjk kdg au tumia ladha yoyote


Chukua bakuli mbili tofauti, moja weka viini vitupu vya mayai, na moja weka ute wa mayai, Anza kuchukua hii bakuli yenye ute tia baking powder yako ianze kusaga kwa speed kubwa kwa kutumia mashine ya kusagia, au kama utatumia mixer ya mkono basi uwe na speed kwenye kukoroga, uku ukiwa unakoroga uku unatia sukari kidogo kidogo mpaka sukari unamaliza endelea kusaga mpaka mchanganyiko wako ujae  uwe mzito kama picha hii👇🏼 itavyokuonyesha


Pizza

UPISHI WA PIZZA

1,,,,MAHITAJI YA UNGA NUSU,,, SUKARI KJK KIMOJA CHA CHAKULA, AMIRA KIJIKO KIMOJA NA NUSU CHA CHAKULA,,, MAZIWA YA UNGA VIJIKO 6 VYA CHAKULA,,MAFUTA YA KUPIKIA VIJIKO 6 VYA CHAKULA, MAJI ROBO TATU KIKOMBE AU PIMA MLS 450,,,,,CHUMVI NUSU KIJIKO KILE KIDOGO,,,,TIA VYOTE KWENYE BAKULI KANDA UACHE UUMUKE

2,,,,MAHITAJI YA ROST,,, NYANYA 4 KUBWA, KITUNGUU KIMOJA,, MAFUTA YA KUKAANGIA,, TOMATO PASTE MOJA,,,, CHUMVI KJK KIDOGO,,,, MENYA NYANYA, ZIKATEKATE, AU ZISAGE,,, KATA KITUNGUU KAANGA, TIA NYANYA, MALIZIA KUWEKA TOMATO NA CHUMVI ROST LIKIWA TAYARI LIWEKE PEMBENI LIPOE,,,

3,,,,KITOWEO UNACHOTUMIA, KAMA PIZZA YA KUKU MCHEMSHE NA VIUNGO AKIWIVA MTOE MIFUPA, MCHAMBUECHAMBUE,,, AU KAMA SAMAKI MCHEMSHE NA VIUNGO AKIWIVA MTOE MIBA MCHAMBUECHAMBUE,,,, AU KAMA NYAMA ICHEMSHE NA VIUNGO IKIWIVA ITOE MIFUPA ACHA STEKI KATA VIPANDE VIDOGOVIDOGO,,,, HALAFU IWEKE PEMBENI,,,

4,,,,,VEGETABLES,,,
KAROT ISAGE,,,,
HOHO KATA VIPANDE VIDOGOVIDOGO
VITUNGUU KATA VIPANDE VIDOGO VIDOGO

5,,,CHEESE AU MOZARELLA

6,,,,UNGA UKISHAUMUKA SUKUMA KAMA CHAPATI LKN UWE MNENE KIASI,,,, UKISHASUKUMA PAKAA ROST LAKO,,, HALAFU ANZA KUWEKA VEGETABLES ZAKO,,, VITUNGUU, HOHO, KAROTI,,,,, UKIMALIZA HAPO WEKA KITOWEO CHAKO,,,, MALIZIA JUU KUWEKA CHEESE,,,, HALAFU IWEKE JIKONI PIZZA YAKO,,, KAMA UNATUMIA OVEN, WEKA MOTO MDOGO CHINI KWANZA MPAKA IKIANZA KUA BROWN MALIZIA MOTO WA JUU DAKIKA CHACHE PIZZA YAKO ITAKUA TAYARI


Kfc kuku

UPISHI WA KUKU WA KFC,,,,
MAHITAJI
KUKU
UNGA WA NGANO(UNGA UTIE CHUMVI KIDOGO, PILIPILI YA UNGA, PILIPILI MTAMA YA UNGA, BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA)
MAFUTA YA KUPIKIA
KITUNGUU SWAUM
TANGAWIZI MBICHI
MAYAI
CHUMVI
NDIMU

MATAYARISHO
1,,,,,OSHA KUKU WAKO,,, PONDA KITUNGUU SWAUM NA TANGAWIZI MTIE KUKU WAKO, TIA NA CHUMVI NA NDIMU,HALAFU MFUNIKE KAMA DK 20 ILI VIUNGO VIKOLEE,, UNAWEZA PIA KUTIA BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA...

2,,,,CHUKUA SAHANI WEKA UNGA WAKO WA  NGANO,,,, CHUKUA BAKULI PASUA MAYAI YATIE CHUMVI KIDOGO(WINGI WA MAYAI INATEGEMEA NA KIASI CHA KUKU)

3,,,,CHUKUA KIPANDE CHA KUKU KICHOVYE KWENYE MAYAI,,,, HALAFU KICHOVYE KWENYE UNGA,,,, KIRUDIE TENA KUCHOVYA KWENYE MAYAI KITIMBUKIZE JIKONI KWENYE KALAI LA MAFUTA,,,, KAANGA MPAKA KUKU AKIWA BROWN TAYARI KWA KULIWA


Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...