Pishi hili maarufu kama Sphagetti bolognese,ni mchanganyiko wa tambi,nyama ya kusaga na njegere(optional).
MAHITAJI:
1. Tambi mfuko mmoja
2. Nyama ya kusaga nusu kilo
3. Nyanya 4
4. Kitunguu swaumu 1
5. Kitunguu maji kikubwa 1
6. Njegere glass ndogo 1
7. Karoti 1 na Hoho 1
8. Chumvi kiasi
JINSI YA KUANDAA:
-Weka mafuta yachemke,kisha kaanga kitunguu swaumu kilichopondwa pamoja na kitunguu maji,hoho na karoti.
-Weka nyama katika mchanganyo huo na ikaange hadi itakapobadilika rangi kuwa ya brown.
-Weka tambi zilizovunjwavunjwa na njegere(zilizochemshwa).
-Koroga kisha ongeza nyanya(ni vizuri zikawa zimesagwa kuliko kukatwakatwa) kisha ongeza maji kidogo.
-Funika acha ichemke,kisha weka chumvi.
-Andaa mezani inaweza kuliwa kama chakula cha wakati wowote,pamoja na kinywaji chochote.
Monday, May 28, 2018
TAMBI ZA NJEGERE
Thursday, May 24, 2018
MKATE WA MAJI
MIKATE YA PILIPILI HOHO/PILIPILI BOGA.
MAHITAJI
maziwa Unga 1/2 kg Kitunguu maji 1 kikubwa Pilipili hoho/boga nyekundu nusu na kijani nusu. Chumvi kiasi Mayai unaweza kuweka 3 ila mimi nimeweka 6 kwa reason zangu mwenyewe, haiharibu kitu ukiweka ma 3 Mafuta ya kupikia.
MATAYARISHO.
Saga kitunguu maji na mayai kwa kutumia blenda (kama huna blender basi visage mpaka viwe laini sana) saga mpaka vitubguu viwe hakionekani, weka unga halafu tia maziwa kidogo kidogo huku unasaga mpaka upate uzito kama kwenye video hapo juu usiwe mzito sana wala mwepesi sana. Ukisha kuridhika mimina kwenye bakuli, kata pilipili hoho vipande vidogo vidogo changanya kwenye unga wako weka na chumvi halafu anza kuchoma mikate yako kwa kutumia chuma
Sunday, May 20, 2018
MKATE WA TURKY
Mahitaji
Unga 3 cups
Chumvi kidogo
Olive oil 2 tsp
Sukari 1 tsp
Maziwa ya maji 1 cup
Maji 1cup
Khamira 1tsp
Yai 1
Laban(mtindi)
Haba souda
Ufuta
🍴🍴🍴🍴🍴
Chukua unga changanya na vitu vyote isipokua yai ufuta laban habasoda
Uchanganye unga wako ukisha changanika vizuri uwache umuke
Ukisha umuka ukate madonge 2 utandaze kama unavyoona kwenye picha chukua uma ufanye kama unautoboa toboa kama hapo pichan unavyouona
Chukua yai ile ya njano tu changanya na Laban (mtindi) kidogo ichanganike vizuri ipake juu ya mikate yako vizuri chukua haba soda na ufuta tupia juu ya mkate wache umuuke tena choma kwa oven uwache uwe rangi kama hapo pichan
🍴🍴🍴🍴
MKATE WA MCHELE
MKATE WA MCHELE/MKATE WA KUMIMINA
Mahitaji
1.Unga wa mchele (rice flour 2
vikombe vya chai)
2.Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha
chai)
3.Hamira (dried yeast 3/4 kijiko cha
chakula)
4.Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko
cha chai)
5.Ute wa yai 1(egg white)
6.Tui la nazi (coconut milk kikombe
1 na 1/2 cha chai)
7.Mafuta (vegetable oil)
MATAYARISHO:-
Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui
la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha
koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu
ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza
kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia
sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada
ya hapo washa oven katika moto wa 200°C
kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake
mafuta na umimine mchanganyiko. Kisha utie
katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40.
Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na
chini. Na hapo mkate utakuwa tayari kuliwa pamoja na chai ya maziwa au ya rangi au hata juice.
NB:-KAMA HAUNA UNGA WA MCHELE WAWEZA CHUKUA MCHELE WAKO NA UKAULOWEKA KATIKA MAJI USIKU MZIMA KISHA UKAUSAGA KATIKA BLENDA NA MKATE WAKO UKATOKA VIZURI PIA.NA KAMA HAUNA OVEN YA KISASA BASI WAWEZA TUMIA JIKO LA MKAA KUOKEA.
Thursday, May 17, 2018
KAIMATI YA SHIRA
Kaimati za sukari ya nje
Maitaji
◾Sukari robo
◾Unga wa ngano nusu
◾Amira kijiko cha chai
◾Iliki kijiko cha chai nusu
◾Samli au mafuta yakukandia
◾Tui la nazi na maji yake ya Nazi
Matayarisho
chukua unga weka kwa bakuli lako
chukua iliki yakusaga weka chukua samli weka au
mafuta chukua Amira iweke kwenye tui lako la nazi
liache kiasi anza kuchanganya unga hadi
uchanganyike tia tui kiasi changanya weka tena ikiwa
Lipo changanya tena ukiona umelainika vizuri weka
yale maji ya nazi chukua mwiko wakupikia sima anza
kuvurugia hadi uwe sawa usiwe mzito sana zikawa
na donge ndani wala usiwe mwembamba zikawa
nyepesi uwe katikati utafutie maali uweke.
Chukua sufuria tia sukari tia maji kiasi bandika jikoni
iache ichemke hadi iive ambapo ukiishika kwa vidole
yanata ukiona ipo hivyo iepue angalia unga wako
umeumuka au ikiwa upo tayari bandika karai lako tia
mafuta mengi ili zichomeke vizuri yaache yapate
moto anza kuchoma hadi umalize.
ukimaliza zitiie kwenye sufuria bandika jikoni moto kiasi
chukua sukari zimwagilie anza kuzipepeta kiasi,
regesha jikoni hadi zishike sukari vizuri
Aandaa tayari kwa kuliwa
PIZZA YA KUKU(CHICKEN PIZZA)
Chicken Pizza
Base
Unga wa ngano vikombe 3
Sukari vijiko 2 vya chakula
Hamira kijiko 1 cha chakula
Baking powder kijiko 1 cha chai
Chumvi kijiko 1 cha chai
Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya chakula
Maziwa kikombe 1
Changanya mahitaji yote kisha kanda mpaka unga ulainike, weka pembeni kwa dakika 30.
Kanda tena kisha kata madonge kwa ukubwa utakayo sukuma duara kisha weka pembeni.
SAUCE
Nyanya 3
Kitunguu maji 1/2
Kitunguu swaumu
Hoho 1/2
Majani ya giligilani
Chumvi
Sukari kijiko 1 cha chakula
Binzari nyembamba ya unga kijiko 1 cha chai
Nyanya ya packet kijiko 1 cha chakula
Weka mahitaji yote kwenye blenda isipokua nyanya ya packet, saga mpaka mchanganyiko wote ulainike.
Weka mafuta vijiko 2 vya chakula kisha bandika jikoni, yakishapata moto weka mchanganyiko wote kwenye sufuria pamoja na nyanya ya packet.
Wacha ichemke mpk ikauke kabisa.
TOPPPING
Kuku, tumia mnofu pekeake.
Chumvi
Pilipili manga kijiko 1 cha chai
Unga wa giligilani kijiko 1 cha chai
Ndimu 1
Vitunguu saumu kijiko 1 cha chai
Tangawizi 1/2 kijiko cha chai
MBOGA MBOGA
Hoho, katakata vipande vidogo
Nyanya, katakata vipande vidogo
Kitunguu maji, katakata vipande vidogo
Cheese (mozarella, cheddar) , kwangua
Katakata kuku vipande vidogo kisha weka mahitaji yote yaliobakia na changanya vizuri.
Weka pan mafuta na yakishapata moto weka kuku kaanga mpk iive kabisa.
Weka base kwenye baking tray, kisha chukua uma uchome chome kwa juu kisha weka sause kwa juu pakaza vizuri hakikisha base yote imekolea, weka cheese kidogo, kisha weka kuku na mboga mboga kisha weka cheese tena kwa juu ya kutosha.
Oka kwenye moto wa 180c kwa dakika 15-20.
Note
Unaweza kuweka sausage badala ya kuku.
PIZZA YA VIAZI(POTATOES PIZZA)
Pizza Ya Viazi
Vipimo
Unga wa ngano - 3 Vikombe vya chai
Chumvi - 1 1/2 Kijiko cha chai
Sukari - 3/4 Kijiko cha chai
Maji - 1 3/4 Vikombe vya chai
Hamira - 1 Kijiko cha chai kilichojaa
Viazi - 2 Vikubwa
Kitungu - 1 kidogo
Mafuta ya Zeituni - 4 Vijiko vya supu
Namna ya kutengeneza na kupika
Changanya unga, 1/2 kijiko cha chai chumvi, sukari, na hamira katika mashine,na mimina maji pole pole.Uwache unga ukandike vizuri hadi ilainike.
Ufunike na uache uumuke kwa masaa 2 au zaidi.
Tayarisha viazi kwa kuzikata slesi na kuziroweka ndani ya maji ya baridi ili isigeuke rangi.
Kisha mwaga maji na uweke chumvi 1/2 kijiko cha chai, iwache kwa dakika 5 hivi ili itowe maji na uyamwage.
Kisha changanya viazi, kitungu kilichokatwa, na mafuta ya zeituni kijiko 1, nauweke kando.
Washa oveni moto wa 440F.Tayarisha trei ya kuchomea kwa kuipaka mafuta.Kisha tandaza unga (uliokwisha fura), ukitumia mikono yako na kusambaza hadi pembeni mwa trei.
Panga viazi, nyunyiza chumvi 1/2 kijiko cha chai, pilipili manga ya unga na mafuta ya zeituni vijiko 3 iliyobakia.
Pika hadi pizza iwachane pembeni na kuwa rangi ya dhahabu, kama dakika 30 hivi.
Epua, na iwache ipowe kidogo;kata vipande na itakuwa tayari kuliwa.
PIZZA YA NYAMA(MEAT PIZZA)
PIZZA YA NYAMA
MAHITAJI
°Unga wa ngano 1/2
°Amila 1/2 kijiko cha chai
°Nyama yang'ombe au kuku 1/2
°Sukari vijiko 1 1/2 cha mchuzi
°Chumvi kiasi
°Nyanya maji 1 kubwa
°Kitunguu 1 kikubwa
°Jibini kiasi
°Olive oil vijiko 2 vya mchuzi
°Maggie 1
°Pilipili manga 1/2 kijiko cha chai
°Karoti 1
°Hoho 1
°Curry 1/2 kijiko cha chai
°Souce ya nyanya
KUANDAA NA KUPIKA
°°° Andaa nyama yako ambayo ni steki kata vipande vidogo vidogo kisha tia katika bakuli au sahani,tia maggie,pilipili manga ya unga,chumvi, curry changanya vizuri kisha tia katika friji viungo vikolee.
°°°Chukua bakuli kubwa weka unga wangano,amila,sukari na chumvi kisha changanya kwa pamoja,mimina maji kiasi na ukande una wako hadi uwe laini kisha weka pembeni uumuke kwa dakika kadhaa.
°°° Katakata kitunguu maji,hoho,karoti na nyanya hakikisha unavikata saizi moja, kwa ngua jibini au isage upate unga wake.
°°° Tizama kama ungawako umeumuka kata kidonge kiasi na usukume round kama chapati,inatakiwa chapati unayo isukuma iwe nyepesi ambapo piza yako itakuwa laini itapokuwa tayari,lakini ukifanya chapati nzito piza itakua ngumu maana ukitia katika oven itaumuka pia.
°°°Baada ya hatua hiyo,chukua nyama yako katika friji,chukua trey ya bati ambayo ni pana paka pafuta ya olive kwa chini kisha nyanyua ile chapati na kuikalisha pale, chukua tena olive paka juu ya chapati,kisha chukua souce ya nyanya paka kwa juu katika chapati yote.
°°°Kisha chukua nyama yako weka kwa juu ukitumia staili ya kusambaza utafanya hivyo pia kwa karoti,hoho na nyanya freshi,na mwisho utamalizia unga wa jibini na olive oil kidogo ili kuisaidia kua laini pia.
°°°Baada ya hapo nyanyua trey yako na itie katika oveni acha kwa dakika 30-35-40 piza yako itakuwa tayari kwa kuliwa na haina muda maalum wa kula wala kupika,pia utafurahia upishi wako.
Fish balls
FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...
-
#biriani #goatbiriani #beefbiriani #birianiyambuzi Mahitaji 1.Mchele wa Basmat 1/2 Kg 2.Nyama ya Mbuzi Stake 1/2 Kg 3.Viazi mbatata viku...
-
Jinsi ya kutengeneza lipbam Aina ya kwanza mahitaji Vaseline /mafuta yoyote ya mgando yani petroleum jelly Mafuta ya Nazi Asali Rangi ...
-
MAKARONI mahitaji makaroni pacti (1) tomato fresh (4-5) kitunguu maji (1-2) hoho (1) karoti (1) maji ya moto kiasi nyama nusu ma...