Thursday, February 20, 2020

Sponge cake part 3

Tutakua tushapata michanganyiko miwili,,,, Hapa Sasa michanganyiko yote miwili imeshakutana kwenye bakuli moja


Tunamimina Sasa kwenye chombo  chetu cha  kupikia, ili tuweke kwenye moto(jikoni)

MOTO 180,dk 35


Part 2 sponge cake

Hatua ya pili Chukua bakuli lenye viini Anza kutia maziwa uku unakoroga endelea kutia mafuta ya kula, pamoja na vanilla koroga mpaka vichanganyike halafu chota unga wa mkono uwe unatia kidogo kidogo uku ukiendelea kuchanganya mpaka vichanganyike vyote,,, tafadhali huu mchanganyiko wa pili USITUMIE mashine yoyote, tumia mixer ya mkono(whisk) au mwiko tu,ukimaliza hapo changanya michanganyiko yako yote sehemu moja,, yaan unachota huo mchanganyiko wa  ute ulosaga kwa kutumia  kijiko unatia kwenye bakuli lenye viini mix vizuri mpaka mchanganyiko wako uwe  sawa


Keksponge

Part1, keki laini ya sponge,,,

Tuangalie Mahitaji kwenye hii keki yetu:

Unga wa ngano gram 150 ambayo ni Sawa na vijiko 10 vya kulia chakula,,,sukari gram 60 ambayo ni Sawa na vijiko vinne mpaka vitano vya kulia chakula,,, mayai manne, maziwa ya maji vijiko 7 mpaka 8, ambayo ni MLS 90 mpaka 100 sio mbaya,,mafuta ya kupikia vijiko 8 ambayo ni MLS 60,,baking powder kijiko kimoja kidogo cha kukorogea chai,, ladha ya vanila kjk kdg au tumia ladha yoyote


Chukua bakuli mbili tofauti, moja weka viini vitupu vya mayai, na moja weka ute wa mayai, Anza kuchukua hii bakuli yenye ute tia baking powder yako ianze kusaga kwa speed kubwa kwa kutumia mashine ya kusagia, au kama utatumia mixer ya mkono basi uwe na speed kwenye kukoroga, uku ukiwa unakoroga uku unatia sukari kidogo kidogo mpaka sukari unamaliza endelea kusaga mpaka mchanganyiko wako ujae  uwe mzito kama picha hii👇🏼 itavyokuonyesha


Pizza

UPISHI WA PIZZA

1,,,,MAHITAJI YA UNGA NUSU,,, SUKARI KJK KIMOJA CHA CHAKULA, AMIRA KIJIKO KIMOJA NA NUSU CHA CHAKULA,,, MAZIWA YA UNGA VIJIKO 6 VYA CHAKULA,,MAFUTA YA KUPIKIA VIJIKO 6 VYA CHAKULA, MAJI ROBO TATU KIKOMBE AU PIMA MLS 450,,,,,CHUMVI NUSU KIJIKO KILE KIDOGO,,,,TIA VYOTE KWENYE BAKULI KANDA UACHE UUMUKE

2,,,,MAHITAJI YA ROST,,, NYANYA 4 KUBWA, KITUNGUU KIMOJA,, MAFUTA YA KUKAANGIA,, TOMATO PASTE MOJA,,,, CHUMVI KJK KIDOGO,,,, MENYA NYANYA, ZIKATEKATE, AU ZISAGE,,, KATA KITUNGUU KAANGA, TIA NYANYA, MALIZIA KUWEKA TOMATO NA CHUMVI ROST LIKIWA TAYARI LIWEKE PEMBENI LIPOE,,,

3,,,,KITOWEO UNACHOTUMIA, KAMA PIZZA YA KUKU MCHEMSHE NA VIUNGO AKIWIVA MTOE MIFUPA, MCHAMBUECHAMBUE,,, AU KAMA SAMAKI MCHEMSHE NA VIUNGO AKIWIVA MTOE MIBA MCHAMBUECHAMBUE,,,, AU KAMA NYAMA ICHEMSHE NA VIUNGO IKIWIVA ITOE MIFUPA ACHA STEKI KATA VIPANDE VIDOGOVIDOGO,,,, HALAFU IWEKE PEMBENI,,,

4,,,,,VEGETABLES,,,
KAROT ISAGE,,,,
HOHO KATA VIPANDE VIDOGOVIDOGO
VITUNGUU KATA VIPANDE VIDOGO VIDOGO

5,,,CHEESE AU MOZARELLA

6,,,,UNGA UKISHAUMUKA SUKUMA KAMA CHAPATI LKN UWE MNENE KIASI,,,, UKISHASUKUMA PAKAA ROST LAKO,,, HALAFU ANZA KUWEKA VEGETABLES ZAKO,,, VITUNGUU, HOHO, KAROTI,,,,, UKIMALIZA HAPO WEKA KITOWEO CHAKO,,,, MALIZIA JUU KUWEKA CHEESE,,,, HALAFU IWEKE JIKONI PIZZA YAKO,,, KAMA UNATUMIA OVEN, WEKA MOTO MDOGO CHINI KWANZA MPAKA IKIANZA KUA BROWN MALIZIA MOTO WA JUU DAKIKA CHACHE PIZZA YAKO ITAKUA TAYARI


Kfc kuku

UPISHI WA KUKU WA KFC,,,,
MAHITAJI
KUKU
UNGA WA NGANO(UNGA UTIE CHUMVI KIDOGO, PILIPILI YA UNGA, PILIPILI MTAMA YA UNGA, BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA)
MAFUTA YA KUPIKIA
KITUNGUU SWAUM
TANGAWIZI MBICHI
MAYAI
CHUMVI
NDIMU

MATAYARISHO
1,,,,,OSHA KUKU WAKO,,, PONDA KITUNGUU SWAUM NA TANGAWIZI MTIE KUKU WAKO, TIA NA CHUMVI NA NDIMU,HALAFU MFUNIKE KAMA DK 20 ILI VIUNGO VIKOLEE,, UNAWEZA PIA KUTIA BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA...

2,,,,CHUKUA SAHANI WEKA UNGA WAKO WA  NGANO,,,, CHUKUA BAKULI PASUA MAYAI YATIE CHUMVI KIDOGO(WINGI WA MAYAI INATEGEMEA NA KIASI CHA KUKU)

3,,,,CHUKUA KIPANDE CHA KUKU KICHOVYE KWENYE MAYAI,,,, HALAFU KICHOVYE KWENYE UNGA,,,, KIRUDIE TENA KUCHOVYA KWENYE MAYAI KITIMBUKIZE JIKONI KWENYE KALAI LA MAFUTA,,,, KAANGA MPAKA KUKU AKIWA BROWN TAYARI KWA KULIWA


Sambusa

SAMBUSA ZA NYAMA
MAHITAJI
1)Nyama nusu(iliosagwa)
2)Pilipili manga kijiko 1 cha chakula
3)Kijiko kimoja cha chakula cha kitunguu Thomu na tangawizi iliyosagwa
4)Mafuta ya kupikia Kiasi
5)Vijiko vinne unga ngano au ute wa yai kwa kufungia sambusa
6)Kaki za sambusa/manda/ chapati nyepesi (unaweza kununua zilizokuwa tayari zimeshakatwa kwa ajili ya sambusa au kama utanunua zile sheet pana utazikata kwa inchi 4 upana wa ruler yaani upate mistari 3
MATAYARISHO
1)Kausha nyama ya kusaga kwa kitunguu swaumu (thomu) na tangawizi pamoja na chumvi mpaka ikauke vizuri Iache ipoe.
2)Kata kata majani ya kotmiri weka upande Kata kata upate vipande vidogo vidogo(chop) vya vitunguu maji.
3)Zikate pili pili zako slice za mviringo vidogo vidogo.
4)Wakati ukimaliza matayarisho haya na nyama yako itakuwa ishapoa kabisa hapo ndio utachanganya,bizari nzima pamoja na pilipili manga pamoja na vitu vyote ulivyokwisha vitayarisha
5)Koroga unga ndani ya kibakuli au ute wa yai
6)Weka kaki kwa mfungo wa triangle yaani pembe tatu kama kofia na weka mchanganyiko wa nyama yako kiasi na uanze kuzifunga sambusa zako na ukifika mwisho hapo ndipo upake unga wako kwa ajili ya kuifunga isifunguke wakati wa kuchoma, pendelea kutumia kaki 2 kwa kila sambusa moja.
7)Kuchoma kwake ikiwa unazifanya na kuzichovya hapo hapo mafuta lazima yawe baridi (ninakusudia uweke mafuta na uzitie sambusa kabla hayajapata moto).Na ikiwa uliziweka kwenye friji zikaganda basi unatakiwa uzichome kwa mafuta ya moto.
NOTE:
Watu wengi hupata usumbufu katika kufunga sambusa, Jaribu mara kwa mara utafanikiwa tu, ni kiasi cha kuzoesha mikono kufuatisha ile Triangle tu.
Pia waweza kutupia njegere kiasi zilizopikwa katika mchanganyiko wako wa nyama ili kupendezesha zaidi.


Halfkeki

HALF CAKE

MAHITAJI
Unga wa ngano  Nusu
Sukari robo
Baking powder nusu kijiko, kile kidogo
Magadi soda (bicarbonate soda)  kijiko cha chai 1,kile kidogo
Mafuta 2 vijiko vya chakula
Mafuta ya kukaangia
Maji ya uvuguvugu kiasi

MATAYARISHO

Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea)kisha ukande(hakikisha unakuwa mgumu)

Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi)

Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke.

Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani.

Zikisha iva zitoe na uiweke kwenye chujio ili zichuje mafuta.

Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.


Mandaz

Maandazi
Mahitaji
1,,,,,, unga kilo moja
2,,,,,,nazi moja tui lijae kikombe
3,,,,sukari nusu kikombe utachopimia tui
4,,,,,,,chumvi robo kijiko kidogo
5,,,,,,,,amira kijiko chakulia chakula kimoja na robo
6,,,,,,,baking poda sio lazima ila ukitaka unaeka robo kijiko kidogo kiasi sawa kama chumvi
7,,,,,,mafuta unayokandia vijiko 6 vya kulia chakula
8,,,,,iriki ilosagwa kijiko kidogo au punjepunje upendavyo mwenyewe,,,
    Ukishachanganya vyote Anza kukanda unga wako ukiwa unaganda mikononi  pakaza unga mikono yako kidogo kidogo uku unaendelea kukanda mpaka uhakikishe unga haunasi mkononi,,, acha unga ukae dk 5 tu alafu Anza kukata maandazi yako, ukishakata yaache kiasi kama cha robo saa au dk 20 inategemea na Hali ya hewa, kama baridi yataitaji muda wa ziada, muhimu tuu yasiumuke Sana yatapasuka jikoni, alafu utaanza kuchoma uku unaligeuzageuza andazi pande zote mbili, unapokata andazi usiliache na nyama nyingi alitoiva ndani, sukuma unga kiasi karibia kama chapati lkn pia usisukume Sana likawa jepesi zaidi litakua kaukau, kua makini kwenye kusukuma ukisie tuu kiasi chakusema lishatosha utaanza kukata


Donught

Doughnut/donut
MAHITAJI
1.Unga – ROBO kilo
2.Sukari-100 grams
3.Mayai  5
4.blueband/Siagi - 4 Vijiko vya chakula
5.Hamira  1 Kijiko cha chakula
6.Baking Powder - 1 Kijiko cha chai
7.Vanilla - 1 Kijiko cha chai
8.Hiliki zilizosagwa -  1 Kijiko cha chai
9.icing sugar– robo kilo
MATAYARISHO
1.Unavunja mayai,unatia sukari,hamira, baking powder,vanilla na hiliki ikisha unakoroga kwa kutumia kikorogeo cha kukorogea keki.Unakoroga mchanganyiko kwa muda wa dakika 5.
2.Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe ya moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko  na unakoroga tena kwa dakika mbili tu.
3.Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa kisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono,mpaka ulainike.
4.Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa,na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.
5.Sukuma na ukate madonge.Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakati ya madonge.
6.Ukimaliza kukata madonge yote,yaweke kidogo yavimbe halafu weka mafuta na uyakaange.
7.Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe yamoto moto kisha yachovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu.
8.Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.


Karanga

KARANGA ZA MAYAI

MAHITAJI
Karanga kilo 1
Yai moja
Mafuta ya kula ( ya maji ) mls 750
Sukari vijiko 6 vya chakula
Unga wa ngano kikombe kimoja cha kahawa( coffee cup)
Chumvi ya unga nusu kijiko cha chai.
Jiko
Chombo –Sufuria/bakuli
Mwiko /kijiko kikubwa

MAELEKEZO

Chukua  yai,  pasua  na  koroga  kwenye  chombo  kisafi. 
Chukua  karanga,mimina kwenye chombo ulicho koroga yai ,changanya kwa kutumia mikono.
Weka chumvikidogo, changanya vizuri, weka sukari changanya, mimina unga wa ngano, changanyavizuri.
Weka mafuta jikoni hadi yapate moto.
Chota karanga kwa kutumia kijiko  kikubwa  na  weka  kwenye  mafuta  kisha  zigeuze  bila  kuacha  hadi utakapoona karanga zimebadilika rangi kua kahawia.
Tumia  kijiko  kikubwa  kuziepua  na  weka  kwenye  chombo  kisafi  cha  wazi  ilizipoe.
Funga kwenye vifuko vidogo na zihifadhi mahali pasafi tayari kwa kula au kuuza.


Kashata

KASHATA ZA NAZI
MAHITAJI
1.Nazi iliokunwa
2.Maziwa (vizuri ukitumia maziwa ya sona ya kikopo ni nzuri zaidi)
3.Hiliki ya unga
4.Siagi kidogo sana kama kijiko kimoja cha chakula.
5.sukari kiasi
6.food color- rangi yoyote(kijani,njano,nyekundu n.k)
MATAYARISHO
1)katika pan weka siagi isubiri ipate moto kidogo.
2)weka rangi, nazi iliokunwa changanya vizuri alafu mimina maziwa,sukari pamoja na hiliki.
3)changanya vizuri hadi ichanganyike alafu ipua.
4)tandaza katika sahani na weka alama za kukata kabisa.
5)weka katika friji ili kashata zishikane
6)kata tayari kwa kuliwa.
NOTE:Kashata zinapendeza kula na kahawa.


Vitumbua

Upishi wa vitumbua
MAHITAJI
UNGA wa mchele nusu(roweka mchele usiku, mpaka asubuhi usage kwenye Brenda, au PELEKA mashine)
Sukari nusu kikombe
Yai moja
Iriki kijiko kidogo
Amira kijiko 1 cha chakula
Mafuta ya kupikia
Unga wa ngano kijiko kimoja
Tui bubu kikombe kimoja

MATAYARISHO
AWAMU YA KWANZA:
Kama unatumia mchele ulioroweka umwage maji utie kwenye Brenda na vitu vyote (kasoro mafuta,) ,,
usage mpaka UHAKIKISHE vimelainika kabisa
Mimina kwenye bakuli UFUNIKE uache uumuke

Ukishaumuka andaa chuma chako cha vitumbua, kiweke jikoni tia mafuta vishimo vyote,,, hakikisha mafuta yamepata moto Anza kuchoma vitumbua vyako,,, baada ya dakika chache pindua juu kuwe chini ili kiwive pande zote

Ukiona kimekua brown tayari unaweza kutoa ili usiunguze kua makini na moto kulingana na jiko unalopikia


AWAMU YA PILI:
kama unatumia unga ulosaga mashine, utie kwenye bakuli na vitu vyote koroga vichanganyike, UFUNIKE mpaka uumuke ndo uanze kuchoma vitumbua vyako

ANGALIZO,,,, kulingana na mchele husika unaotumia ukiona uji wako mzito zaidi, ongeza VIMAJI kidogo maana uji ukiwa mzito Sana vitumbua haviwivi ndani


Bagia

AWAMU YA KWANZA
BADIA ZA DENGU SIMPO HAZINA MAMBO MENGI
UNGA WA DENGU NUSU
UNGA WA NGANO ROBO KIKOMBE
CHUMVI KIJIKO KIMOJA
BAKING POWDER KIJIKO KIMOJA KIDOGO

MATAYARISHO

CHANGANYA VITU VYOTE KWENYE BAKULI TIA MAJI NUSU KIKOMBE UKIONA MZITO SANA ONGEZA KIDOGO
ZIFUNIKE NUSU SAA ANZA KUCHOMA KWENYE KALAI LA MAFUTA MPAKA UKIONA ZINAKUA BROWN ZITAKUA TAYARI

AWAMU YA PILI BADIA ZA DENGU(ZA KIHINDI)

MATAYARISHO
CHANGANYA VITU VYOTE KAMA HAPO AWAMU YA KWANZA,,, HALAFU ANZA KUTIA VITUNGUU ULIVOKATA VYEMBAMBA VIREFU,,, KAROTI ILOSAGWA,,,, HOHO KATA JEMBAMBA KAMA SAIZ YA VITUNGU HIVYO HIVYO,,,, VIAZI KATA MUUNDO WA CHIPS LKN VYEMBAMBA SANA,,, UKIPENDA TIA PIA BILNGANYA NALO KATA KAMA ULIVOKATA VIAZI,,, UTATIA PILIPILI MTAMA YA UNGA, BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA NA NZIMA NZIMA, PILIPILI YA UNGA KAMA UKIPENDA, BIZARI YA NJANO,, KOTMIR,,, UTAMIX VITU VYAKO VYOTE KWENYE BAKULI LENYE UNGA WAKO WA DENGU UTAFUNIKA BAADA YA NUSU SAA UTAANZA KUCHOMA KWENYE KALAI LA MAFUTA YA MOTO


Kach

Upishi wa kachori
MAHITAJI TUNAYOTUMIA KWENYE KACHORI NDIO HAYO HAYO TUNATUMIA KWENYE KATRES ILA KWENYE KATRES KINACHOONGEZEKA NI NYAMA AU SAMAKI INATEGEMEA NA AINA YA KATRESS ZAKO,,,, PIA NDIO MAHITAJI HAYO HAYO TUNATUMIA KWENYE EGGCHOPS ILA EGGCHOP NDANI KUNAWEKWA MAYAI YALOCHEMSHWA

AWAMU YA KWANZA KACHORI

CHEMSHA VIAZI KILO MOJA MPAKA VILAINIKE
VIKIWIVA VIPONDEPONDE, KAMA ULICHEMSHA NA MAGANDA YATOE KWANZA,,,,,
UKISHAVIPONDA VITIE CHUMVI KIJIKO KIMOJA UNAWEZA KUONGEZA KIDOGO (UTAONJA)
HALAFU WEKA PILIPILI YA UNGA, NDIMU, BIZARI NYEMBAMBA YA UNGA, KAROTI ILOSAGWA, HOHO LILOKATWA VIPANDE VIDOGO VIDOGO,,, KITUNGUU MAJI KILICHOKATWA VIPANDE VIDOGOVIDOGO, PILIPILI UKIPENDA MBICHI SAWA TU SIO LAZIMA YA UNGA,,
KAMA UNA MAJANI YA KOTMIR PIA WEKA JAPO SIO LAZIMA,,
KITUNGUU THOUM NA TANGAWIZI VIWE VYA UNGA AU KAMA VYAKUPONDA BASI VILAINIKE VIZURI

VITU VYOTE UTACHANGANYA HUMO KWENYE VIAZI, HALAFU UTAANZA KUVIRINGA DUARA MPAKA VIAZI VYOTE VIISHE

HATUA INAYOFATA CHUKUA UNGA WA NGANO UTIE KWENYE BAKULI TIA MAJI UPATE UJI MZITO UKIWA MWEPES KACHORI AISHIKANI
UKISHATIA MAJI UNGA WAKO TIA CHUMVI KIDOGO,,, NA BIZARI YA NJANO AU RANGI YOYOTE UTAYOPENDA,,,,

CHOVYA DONGE MOJA MOJA KWENYE UNGA UTIE JIKONI KWENYE KALAI LA MAFUTA,,, BAADA YA DAKIKA CHACHE UTAKUA UMESHAPATA KACHORI YAKO


Katr

AWAMU YA PILI KATRESS
KAMA NILIVYO SEMA MAHITAJI YOTE NDIO HAYO HAYO ILA HAPA TU KISHA CHANGANYA VITU VYOTE KWENYE VIAZI TUNATIA NA NYAMA YA KUSAGA AU SAMAKI ALIECHAMBULIWA HALAFU NDIO TUNAANZA KUVIRINGA MADONGE NA KWENYE KUCHOVYA ATUTUMII UNGA WA NGANO KAMA KWENYE KACHORI HAPA TUTACHOVYA KWENYE BAKULI LENYE MAYAI NDO TUTACHOMA JIKONI,KWENYE KALAI LA MAFUTA MPAKA ZIKIWA BROWN KATRESS ZAKO TAYARI


AWAMU YA TATU KWENYE EGGCHOPS
MAHITAJI NI YALE YALE ILA HAPA TUNATAKIWA TUWE NA MAYAI YAKUCHEMSHA YAKUTOSHA

KATA VIPANDE VIWILI AU VINNE KILA YAI(INATEGEMEA NA UKUBWA WA EGGCHOPS ZAKO)

CHUKUA VIAZI MKONONI KABLA UJAVIRINGA PACHIKA KIPANDE CHA YAI HALAFU VIRINGISHA VIAZI VIFUNIKE YAI,,,, UTACHOVYA KWENYE MAYAI KAMA TULIVOFANYA KWENYE KATRESS,,,, UKIKOSA MAYAI UTACHOVYA KWENYE UNGA WA NGANO KAMA ULE ULE WA KACHORI

JAMBO MUHIMU LA KUZINGATIA

KUNA BAADHI HUPENDA KUTUMIA BREADCRUMBS KAMA UTAPENDA,,,, BASI TUMIA KUCHOVYA KWENYE MAYAI HALAFU CHOVYA KWENYE BREADCRUMBS NDO UCHOME JIKONI,,,,, NJIA HII UKITUMIA KWENYE P KACHORI PIA USITUMIE UNGA WA NGANO TUMIA MAYAI KUCHOVYA KAMA KWENYE KATRESS

BREADCRUMBS NI CHENGA CHENGA ZA MKATE ULIOKAUSHWA UKAPONDWAPONDWA


Vish

.Visheti vya kokoto
MAHITAJI
siagi robo
Sukari robo
Maziwa ya unga vijiko 2 vya chakula
Baking powder kjk 1cha chakula
Unga wa ngano nusu
Yai 1
Vanilla au ladha yoyote kijiko 1
Mafuta ya kupikia nusu lita

MATAYARISHO

Saga sukari na siagi pamoja mpaka ilainike weka yai.
mix vizuri halafu weka unga, vanila kijiko kimoja, baking powder na unga wa maziwa changanya vizuri.
weka maji kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wako mpaka uwe donge moja USIJAZE maji  na wala usiwe mgumu sana.

Ugawe madonge  8
chukua kila donge sokota kama kamba na ukate vipande vidogo vidogo dizain ya kokoto,,

weka mafuta  jikoni yakipata moto weka visheti vyako  mpaka viive visiwe vyekundu sana.
toa viweke pembeni vipoe.

MATAYARISHO ya shira
👇👇
Weka sufuria  kwenye jiko weka maji kikombe kimoja na sukari kikombe kimoja, acha ichemke mpaka iwe nzito

utaona inaaza kuganda pembeni mwa sufuria
weka vanilla na visheti punguza moto uwe mdogo
Mix mpaka viwe vikavu kabisa (vizuri kuvi mix kwa kuliinuwa sufuria  na kuvipeta ili visivurugike). Tayari kwa kuliwa


Kalimat

Kalimat
Mahitaji
1,,,,unga ngano nusu
2,,,,unga wa mchele vjk 2 vya chakula
3,,,,chumvi kjk kidogo
4,,,,amira kjk 1 cha chakula
5,,,,sukari kjk 1na nusu cha chakula
6,,,maziwa au tui vjk 2 vya chakula
7,,,mtindi vjk 3 na nusu vya chakula
8,,,,corn flour vjk 3 na nusu vya chakula

MATAYARISHO

Vitu vyote hivyo Tia kwenye bakuli halafu Anza kunyunyizia maji uku unapiga mpaka iwe laini, kisha Tia mafuta vjk 3 na nusu endelea kupiga, sjakupa kiwango cha maji kwahiyo unatakiwa uku unatia maji  uku unaangalia mpaka ukiona uji ushakua mzito mzito piga mpaka uone vipovu, ukimaliza tuu kupiga Anza kuchoma usiusubiri uumuke, Kadri utavokua Unachoma ndivyo vitavokua vinazidi kuumuka kwenye bakuli


UKIHITAJI shira tumia iyo iyo tulotengeneza hapo kwenye visheti


Jicho

JICHO LA NGAMIA

MAHITAJI

SAMLI AU BLUE BAND GR 200
MAYAI 2
BAKING POWDER KJK 1 KDG
ICING SUGAR NUSU KIKOMBE(GR 125)
VANILA KJK 1 KDG
UNGA GR 500(NUSU)
CORN FLOUR GR 125(NUSU KIKOMBE)

MATAYARISHO

CHANGANYA VITU VYOTE KWENYE BAKULI,,,

MCHANGANYIKO UKIWA TAYARI CHOTA MKONONI ZUNGUSHA VIDUARA VIDOGO VIDOGO PANGA KWENYE MASHINE YAKO,,,,,

FUNIKA KWA DK CHACHE TUU HALAFU FUNUA VITAKUA TAYARI,,,,

USIVIACHE MUDA MREFU VITATOKA VIGUMU

UKISHAVITOA VISAWAZISHE PEMBENI KWA KUTUMIA KISU ALAFU PAKAA  CONDENCED MILK AU  NUTTELA MULE ULIPOSAWAZISHA, CHUKUA KINGINE GUSANISHA VIGANDANE,,, JICHO  LA NGAMIA LITAKUA TAYARI

KUNA WENGINE MULE NDANI HUWEKA ROSE AU NJUGU AU KOROSHO, NI HIYARI YAKO SIO LAZIMA


Upishi wa skons

SKONS

MAHITAJI

UNGA KILO MOJA
MAYAI 2
MAFUTA NUSU KIKOMBE
SUKARI KIKOMBE 1
MAZIWA MOTO KIKOMBE 1
MAJI MOTO VIKOMBE 2
SAMLI KJK 1
CHUMVI KJK KDG 1
AMIRA VJK 2

MATAYARISHO

1,,,TIA AMIRA KWENYE MAZIWA DK 5 IACHE IYAYUKE,,,, HALAFU MIMINA MAZIWA NA MAFUTA KWENYE BAKULI LENYE UNGA CHANGANYA KWA MKONO MPAKA UNGA WOTE UENEE MAZIWA NA MAFUTA.

2,KWENYE BAKULI LENYE UNGA,,, MIMINA MAJI, TIA SUKARI,, TIA SAMLI, CHUMVI, TIA VIINI TU VYA MAYAI, UTE UACHE,,
CHANGANYA KWA STYLE YA KUKANDA, KAMA UNATUMIA MIKONO SAWA AU MASHINE NI WEWE TU MWENYEWE,,,,

3,,KANDA KWA MUDA USIOPUNGUA DK KUMI MPAKA 15 HAKIKISHA UNGA UMEKUA MLAINI HAUNASI MIKONONI,, UFUNIKE ROBO SAA MPAKA DK 20.


4,,BAADA YA HUO MUDA KUISHA, FUNUA UNGA WAKO NA UUKANDE TENA DK 5,,,,HALAFU ANZA KUKATA MADONGE KWA SAIZ UPENDAYO,,, PANGA KWENYE CHOMBO CHAKO CHA KUPIKIA

5,,,MADONGE YAACHE YAUMUKE MUDA USIOPUNGUA DK 15 MPAKA 20,,,,WAKATI UNASUBIRI MADONGE YAUMUKE WASHA OVEN LAKO MOTO 150,,,, AU 140 INATEGEMEA NA SPEED YA OVEN LAKO MOTO UWE FULL JUU NA CHINI(KAMA UNATUMIA MKAA KOLEZA MOTO ILI UFUNIKIE JUU NA CHINI)

6,,,MADONGE YAKISHAUMUKA PAKAA UTE WA MAYAI JUU, KAMA UKIPENDA PIA WEKA UFUTA,,, HALAFU WEKA JIKONI KWA MUDA USIOPUNGUA ROBO SAA HAPO UWE MAKINI KUANGALIA USIUNGUZE,,,,, SKONS ZAKO ZIKISHA KUA TAYARI UKIZITOA TU JIKONI ZIPAKAE MAFUTA YA KULA JUU LKN SIO MENGI, TUMIA BRASH KAMA UNAYO, KAMA HUNA CHOVYA KWENYE KITAMBAA KISAFI PAKAA JUU JUU ZIACHE ZIPOE ZITAKUA TAYARI KWA KULIWA


UKIHITAJI KUTUMIA UNGA NUSU, VIPIMO VYOTE UTAVIGAWA NUSU YAKE


Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...