Monday, July 31, 2017

WAKATI NI UKUTA

Kuna baadhi yetu hua tunajisahau sana kwa kuhisi labda apa tulipo ndo tumeshafaulu maisha,hatukai tukajiuliza kwamba kuna kesho tunahitaji kujenga familia kama walivoishi wazazi wetu,

Ni misingi mizuri ikiwa utakaa japo dk kumi ukajitafakari ulikua wapi?upo wapi?na unaelekea wapi??ukipata muda wakutafakari hilo utaelewa maana yangu,,,,,

WAKATI NI UKUTA usije kustuka muda ushapotea unaishia kuangalia maisha ya wenzio na familia zao,,,,,,

Ndipo unaanza kutamani kua na familia ukiangalia umri umeshakutupa,maisha umeshayachezea,kila kitu kipo tofauti na matarajio

Amsha akili yako kwa kuonea wivu wenzio,kwanini wao waweze wewe ushindwe?utakua ni ulimbukeni wa akili kwa kusindikiza wenzio kila siku

Hata vitabu vya dini viliandika muda ukifika unatakiwa ujenge familia kwa kuoa/kuolewa

Starehe zina mwisho wake,ujana una kikomo chake,lkn pia ukumbuke umri nao una mwisho wake,,jaribu kutafakari,,,,,,,


FAIDA ZA UNYWAJI JUICE HIZI 3 TOFAUTI

Inawezekana ukawa unajua,lakini sio mbaya nikikujuza zaidi,,,tuangalie faida tunazozipata ktk juice hizi tatu kiafya,,,,,

1,,juice ya nyanya,,imezoeleka kwamba  nyanya ni kiungo mama kwenye mboga zetu tunazopika kila siku,lkn pia ni kiungo kwenye kachumbari,,je unajua faida yake ikiwa utaifanya kua juice?,,,hii ni nzuri zaidi kwa kinamama kwa sababu inasaidia kuzuia tatizo la saratani ya matiti,,

tunda la nyanya lina madini aina ya lycopene ambayo ni kemikali za mimea zinazozuia saratani kwa kiwango kikubwa sana,,

2,,juice ya nanasi,,hutumika kusaidia kuweka sawa mapigo ya moyo yanayoenda kwa kasi,,

,juice ya nanasi ina madini ya chuma,,,na pia tumezoea kuona karoti ndio tunda kuu ktk usafishaji wa macho,lkn pia nanasi lina nguvu kubwa ktk kuleta nuru ya macho na kuzuia maambukizi madogomadogo ya maradhi katika mwili

3,,,juice ya apple,,,katika kila tunda tunaona kuna upatikanaji mkubwa wa vitamin c,ikiwemo apple,,

lkn pia ikumbukwe kua juice ya apple husaidia kupunguza mwili, Ina viondoa sumu vya mwili (anti oxidants )hivyo inasaidia mtu kupunguza uwezekano wakupata cancer,,magonjwa ya moyo na sukari,,,,kuna faida nyingi sana endapo tutakula matunda kiufasaha,,,kaa nami mambo mazuri zaidi yanakuja,,,,,


Friday, July 28, 2017

OGOPA SANA CHOZI LA MWANAMKE

Hili linajulikana wazi halina ubishi,asilimia kubwa sana ya wanaoongoza kwa uvumilivu kwenye mahusiano/ndoa ni wanawake

Hii ni kutokana na mioyo ya uvumilivu waliopewa na mungu,,

Simaanishi kwamba wanaume hawana uvumilivu laa,,,,wanao uvumilivu tena  sana lkn asilimia zao zipo chini tofauti na mwanamke


Mwanamke ana uwezo wa kudumu na mume mlevi ata miaka 50,ana uwezo wakukufumania ata mara mia na bado akakusamehe,

Anaweza kuishi na mwanaume mpigaji yeye kila siku mwili wake ni kama ngoma lkn bado akakusamehe

Utadumu nae miaka mingi kutokana na uvumilivu wake lkn tambua ya kwamba machozi yake ni sumu kubwa kwenye maisha yako

Jaribuni kua waelewa wanaume,na hasa nyakati izi tulizonazo za utandawazi,,usijaribu kuuchezea sana moyo wa mwanamke hiyo ni laana


Atakuvumilia sana,atateseka sana na hiyo yote ni kwa sababu ya mapenzi yake ya dhati alonayo kwako

Lkn siku atakayoamua kusema basi,ile basi yakutoka moyoni basi ujue ndio basi

Ngumu kuurudisha moyo wake nyuma sana sana anaweza ata kukuwekea sumu kwenye chakula ambacho mtakula pamoja ili mfe wote

OGOPA SANA CHOZI LA MWANAMKE


Friday, July 21, 2017

JIFUNZE KUIMARISHA FURAHA YAKO

Inakuaga ni siku ya furaha sana na hujihisi ni pekee mwenye bahati kwenye dunia kwa mungu kukuunganisha nae,

lkn cha ajabu furaha hutawala kipindi kifupi sana kwa wengi wetu,

ni wachache sana wanaodumu na hii furaha kwenye ndoa zao

Haimaanishi labda hukujipanga kua nae,umeshinikizwa?jibu linabaki hapana,kwanini hapana?ulifanya maamuzi sahihi kwa kujua sasa nina mtu sahihi

Jambo lakujiuliza ni kwa nini sasa hii furaha isiendelee?nini kikwazo?ikiwa mlikubaliana na mkawa na lengo moja lakuungana kua mwili mmoja?


Asilimia kubwa mie husema ni ushetani tuu unaopita kati yenu,siku zote adui wa ndoa zote ni shetani,kwanini mumpe nafasi shetani?ikiwa mnamjua vizuri hapendi kuona watu wakiwa pamoja na furaha zao kwenye ndoa

Muepuke na kama hujui njia za kumuepuka fuata haya yafuatayo


Kwanza kabisa mtangulize Mungu kwa kila kitu,,pili jaribu kua karibu na wazazi pande zote mbili ili hata zikianza dosari wazee wawe na nguvu yakusolve coz wao ndio ngao yako siku zote


Tatu,epuka marafiki wanafki na hasa upande wa mwanamke,,hii ipo pande zote ata upande wa mwanaume pia anao marafiki wanafki lkn kuna unafuu wa kustahmili mikiki kwa mwanaume tofauti na wanawake mioyo yao miepesi


Jiwekee kiapo cha nafsi kwamba ndo huyu huyu simuachi hata iweje,nimeshamvaa na siwezi kumvua kamwe kwenye shida ntakufa nae na kwenye ntakula nae


Maongezi mazuri mdomoni na tabasamu la usoni siku zote za maisha yako


Upole,unyenyekevu,kujali,hisia zake ziwe zako muda wote awepo au asiwepo,,kila gumu analopitia mnasolve pamoja kwa kupeana moyo


Huruma pindi mmojawapo amekwama,sio kipindi cha raha unafurahika akikwama tuu unambadilikia hiyo haitakujenga kamwe


Jitahidi sana kubuni mbinu mpya kila siku ili asikuone yule yule tuu,,ajaribu kukuona mpya kila siku za maisha yake



Pendeleeni kutoka pamoja nyakati za jioni,tembeleeni ndugu na jamaa,wazazi na hata wagonjwa mahospitalini ili mpate baraka zao

Yapo mengi ili kuidumisha furaha yako ndani ya ndoa yako lkn kwa leo naishia hapo tukutane wakati ujao


Tuesday, July 18, 2017

AINA NNE YA VYAKULA MUHIMU

VYAKULA VYA AINA NNE VINAVYOWEZA KU DETOXIFY TUMBO LAKO BILA SHIDA

_________________
🍋Machungwa: !
Yanaweza kukusaidia kusafisha tumbo lako na kukufanya urelax kwakurahisisha mmeng'enyo wa chakula katika tumbo.Kutokana na vitamin C na alkaline inayopatikana katika machungwa inasaidia katika kupigana na bacteria tumboni pamoja na kuongeza kinga zako za mwili.
________________________
🍃Vitunguu swaumu:
!
Vinasaidia pia katika kusafisha tumbo kwa wepesi hasa kwa watu wenye parasites pia ni vizuri katika kulinda tumbo against bacteria,fangasi na virusi vya aina mbalimbali.

_____________
🍇Nazi:
!
Zinasaidia kuua parasites katika mwili hasa katika mfumo wako wa kumeng'enya chakula.Unaweza ukatumia mafuta ya nazi kama nilivyoyaelezea katika post za nyuma na si lazma nazi yenyewe kama tunda na yatakusaidia ku cleans mwili wako kwani yana faida nyingi kama nilivyozieleza.

_______________
🍓Strawberries:
!
Zinafanya kazi kama machungwa yanavyofanya kazi.Zina high antioxidant inayosaidia katika kupigana na bacteria na virusi katika tumbo.Pia zinasaidia kuongeza kinga ya mwili wako na kukulinda na magonjwa tofauti tofauti kama cancer. :
:
________________
🍎🍎Kama una tumbo ambalo haulielewi ni vizuri ukaanza kufanyia kazi hizi dondoo


Sunday, July 16, 2017

BADILISHA AKILI

HAKUNAGA SIRI KATI YA WAPENZI

Ukiona imeanza tu password inabadilishwa badilishwa, simu inaongelewa pembeni, meseji zinafichwa ujue kuna kitu kichafu kinaendelea.

Wengine ndo wanafikia hatua ya kubakiza vitu vya wapenzi wao wa nyuma au kujifanya wana urafiki tu.  Ni nyoka wazuri tu wanasubiri muda muafaka wakung'ate

Mapenzi ni furaha, utani, jokes, tip kissings, romance, umoja, kushirikiana in success, kushikana mikono msianguke, kuicheka dunia,  kuumia na kufurahia wote maisha, ni kuwa na amani ya kuwa mwili mmoja au kitu kimoja.

Haiwezekani asikutambulishe,  asikuheshimu.

Tambua thamani yako.Respect your dignity. You cant b with low life loosers, akileta dharau,
Usifanye kama yeye utakua upo level moja na yeye.

Akileta ujinga mruhusu akafanye ujinga na wajinga wenzake. Haitaacha kukuuma ila ukijithamini watakuja wenye hadhi yako. Utachagua yupi umruhusu.  Na watakuthamini.

Usirudi kwa makombo au mtu yeyote aliyechezea nafasi. Hata kama anasema amebadilika, ukirudi unajivua nguo.

Kubali kuumia, potezea upuuzi. Dunia ina watu wazuri wanajiheshimu na wanatafuta mtu kama wewe.

You deserve better


UTANI HUZIDISHA UPENDO

UTANI HUIMARISHA UPENDO
Jizoesheni kutaniana pindi mnapokua faragha,utani una nafasi kubwa sana kwenye kuzidisha upendo lkn usizidi mipaka ikapelekea ule utani kusababisha mmoja wenu akachukia

Si vizuri kuishi ndani kama mazimwi,na hii ni asilimia kubwa kwa wanaume pirika za utaftaji hupelekea kua seriosly sana hata akiwa na mwenza wake chumbani

Hujikuta muda wote kakunja sura hali inayopelekea hata mke kuogopa kuanza kumtania,jaribu kukunjua paji lako la uso pindi tuu uanzapo kuona kibaraza cha nyumba yako

Usimkunjie uso sana mwenza wako kiasi kwamba mida ikikaribia kurudi nyumbani anaanza kuingia unyonge kwa kufikiria unavomkunjiaga sura kila siku

Na kwa upande wa wanawake pia jitahidi sana kumchokoza mwenza wako kwa viutani vidogo vidogo ata kama alikua na uchovu wa kazi za kutwa nzima ajiskie nafuu kutokana na jokes za hapa na pale

Kingine pia mwanamke anaweza kua chanzo cha mume kua na hali hiyo ya kisrani kila arudipo nyumbani kutokana na visa na kero unazomfanyia

Jaribu kua mcheshi kwa mwenzio kiasi kwamba ata akiwa kazini awe anaona kama saa haziendi ili awahi kurudi nyumbani mapema kutokana unakua unamfanya ajiskie vizuri kwa vijokes vyako vya hapa na pale

Mwanamke jiweke msafi muda ote na hasa manukato mazuri yazidi kipindi ambacho unajua mida hii mume anarejea nyumbani,ili ile hali yakumfanya akuchukie kwa kiharufu kibaya isiwepo


Hiyo points ya usafi ni mojawapo ya sababu nyingi kwa wanaume kua na visrani nyumbani mana hana raha,anaingia unyonge mida ya kurudi ikifika ikiwa tuu anawaza hali atayoikuta uko nayo


Nitaizungumzia zaidi kwenye kipengele kingine cha usafi kwa wote wawili kwa wakati mwingine lkn leo hii tuangazie hapo kwenye mada husika ya kutaniana


Thursday, July 13, 2017

NG'ARISHA USO KWA MASK NZURI YA YAI NA YOGHURT

Kwa wale wenye tatizo la chunusi sugu usoni,nimewaletea mask nzuri na nyepesi unaweza kuifanya ukiwa nyumbani kwako,mchanganyiko wa ute wa  yai na yoghurt utakusaidia sana kuremove chunusi na kung'arisha uso,,,

Egg Whites&Yoghurt Mask
Ingredients:
2 egg whites, separated from the
yolk and placed in a bowl
2 tablespoons of plain yogurt (I
like Greek yogurt)
Preparation:
Separate the egg whites from a
couple eggs and place them in a
bowl. Add 2 tablespoons of yogurt
(do not use flavored yogurt!). Mix
them up and apply to face. Leave on
face for a few minutes then rinse
face in warm water

Kwa mask,facial,scrub natural nyinginyingi unaweza kupitia kwenye blog yangu kwa kugonga link juu hapo juu☝


UKWELI HUMUACHA MTU HURU

UKWELI HUMUACHA MTU HURU,,,

Unapoamua kuingia kwenye mahusiano jitahidi sana kua mkweli,siku zote mapenzi ya kweli hua hayachagui,kua mkweli tuu kwa mwenza wako hata kama unalala chini muelezee tuu kama ameshaamua kukupenda hatolijali hilo,

haina haja yakuazima chumba cha mshkaji wako ukijiachia eti na kujiona upo juu huo ni uboya,kama hauna hata baiskeli kua mkweli tuu we mwambie sina ata baskeli lkn nimekupenda,


kama ameamua kukupenda hatolijali hilo lkn unapoazima gari la rafiki yako kumbuka njia ya muongo fupi,kuna haja gani yakujisumbua akili kwa vitu vya kuazima?pambana na hali yako,,

Itakua siku zote unatumia njia za udanganyifu ili kuwapata kina mwajuma,na unawapata kweli kwa kua nia yao ni kutaka mwanaume anaeonekana anazo,lkn kuna siku utajikuta unaangukia kwa mwanamke mwenye akili zake timamu,mwenye msimamo wake,ambae alijitolea tuu kukupenda vyovyote ulivyo lkn akigundua uongo wako anakuacha mchana peupee,,

Pambana na hali yako

Mwambie tuu ukweli,usifiche ata kama unalalia mkeka we mwambie tuu pengine ujio wake ndio utakaokufanya ukapata baraka ata kuambulia kupata godoro ili muanze maisha


Pambana na hali yako

Uongo haukusaidii kitu na njia ya muongo fupi siku zote,ukweli hukuacha huru na kuishi kwa amani


Lkn ukiishi kwa  uongo huwezi kua huru,huwezi kua na amani,utaishi kwa kujificha ficha ili kuficha aibu yako

Mwanamke akiamua kukupenda hata ukimwambia unalala kwenye duka likishafungwa mie naamini mtalala pamoja kama walinzi mpaka mtapofanikiwa kupata chumba chenu,lkn ukitumia uongo utajikuta kuna siku unaipoteza lulu iliyokuja kumulika maisha yako bila ya kutegemea

Pambana na hali yako


NJIA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO

NAMNA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO

Katika somo hili nakuletea mbinu rahisi kabisa ya kung’arisha meno yako na yakaonekana meupe na yenye kupendeza.

Unahitaji vitu viwili, limau na baking soda au wengine huiita bicardonate of soda nayo ni ile wamama huitumia wanapopika maandazi au mikate, inapatikana maduka ya kawaida hata kwa Mangi hapo nje ipo.

Namna ya kuandaa:
Chukua limau kubwa moja ikate katikati, chuja kupata maji maji yake (juisi) kisha changanya baking soda ya unga kijiko kidogo kimoja cha chai. Changanya vizuri mchanganyiko huo.

Sukutua kinywa chako vizuri ukitumia mswaki na huo mchanganyiko ndiyo iwe dawa yako ya meno. Sukutua (piga mswaki) taratibu kama dakika 3 hadi 5 hivi na mwisho jisafishe kinywa na maji safi.

Mhimu: Fanya zoezi hili nyakati za jioni au usiku unapokaribia kwenda kulala na ufanye mara moja tu kwa wiki na si zaidi ya hapo kwani unaweza kuharibu fizi zako kwa dawa hii usipokuwa makini.
Njia hii pia haisaidii kwa wale ambao wamezaliwa na meno ya rangi hivyo au kama matokeo ya kutumia maji yenye madini kwa muda mrefu kama vile watu wa mikoa ya Arusha au Moshi.

Ukifanya hivi mara 2 au 4 yaani mwezi mmoja utaona tayari meno yako yameanza kuwa meupe na yanayong’aa na kupendeza.

Vyakula kadhaa vifuatavyo vinasaidia kung’arisha meno yako navyo ni pamoja na machungwa, strawberry, mapeazi, maziwa, mtindi, maji ya kunywa, jibini (cheese), broccoli, celery, karoti, tufaa (apple), kitunguu maji, mbegu mbegu (kama korosho, karanga, almonds) nk .

Vyakula au vitu vinavyoharibu rangi ya meno ni pamoja na uvutaji tumbaku au sigara, chokoleti, chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine baridi vyenye kaffeina.


Wednesday, July 12, 2017

FAIDA ZA KULA TIKITI MAJI

Kula TIkiti Maji Kwa Afya Yako


Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.


Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.


Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:


Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.


Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.


Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake.


Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.


Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.


Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.


Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra.


Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.


Kwa kawaida tunda hili huliwa peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.

Huimarisha misuli, Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini


ZINGATIA VITU VITATU ILI UDUMU NA MWENZA WAKO

Inawezekana alishakutana na wengi wazuri,wenye sifa,muonekano na uwezo wa kila kitu lkn hakudumu nao,

Hii sio kwamba hawakumpendeza,sio kwamba hakuwapenda,sio kwamba hakupanga malengo yakuishi nao,ila tuu ni kutokana na wao hawakujua kutunza vitu muhimu vitatu

Unapoamua kuanzisha nae mahusiano unatakiwa ujiwekee ndoto kwenye akili yako ya kwamba huyu ndie chaguo langu na ndie ntazeeka nae

Lkn kama ukiingia kwa mguu mmoja ndani mmoja nje hautajiwekea hiyo ndoto akilini kamwe,utakua mtu wa kusua sua tuu bila mpangilio maalum huku ukishuhudia watu wakimaliza miaka kwenye ndoa zao,


Kanuni kuu ya kudumu nae ni kusema na hivi vitatu kwanza
1...moyo
2...mdomo
3...macho

Hivi vitu vitatu ni vitu vya kuviogopa sana,kwa sababu ndio vitu vikuu vinavyotuponza kila siku kwenye maisha yetu,

Chunga sana moyo wako usije ukabadili msimamo wako kwa umpendae ukajikuta moyo unaangukia kwingine kumbe ni tamaa tuu kule wala hupendwi unakwenda kupoteza muda wako tuu kwa kudanganywa huku ukimuacha yule muhimu ambae alikupenda kwa dhati,,

Chunga sana mdomo wako,mdomo ndio unaoongoza kuponza wengi kwenye mahusiano/ndoa,kabla hujaongea anza kufikiri kichwani kwanza je!hiki nnachotaka kuongea kitampendeza mwenzangu?ukiona kina hitilafu ni bora kuacha,maana siku zote kuna msemo usemao ni bora kukaa kimya kuliko kuongea mpaka unyamazishwe,,mahusiano yaliyo bora hayaitaji mdomo kuongea sana yanahitaji matendo tuu yakuonesha ni jinsi gani unakubali juu ya uwepo wake kwako,,,


Chunga sana macho yako,na hasa mnapokua sehemu za watu,acha kukodolea macho visivyokuhusu mbele yake hiyo ni mbaya na inaweza kukushusha haraka bila mwenyewe kujijua,,,


Maarifa yako yamo ndani ya akili yako,,jichunguze je!upo makini ktk ivyo vitu vitatu???

Jikosoe na ujibadilishe utaamini nnalosema na mtadumu miaka yote


Tuesday, July 11, 2017

AINA SABA YA MATUNDA YANAYOSAIDIA KUKATA MAFUTA TUMBONI

KUPUNGUZA MLUNDIKANO WA MAFUTA TUMBONI


Tuangalie kwa umakini sana njia saba ambazo huondoa haraka mafuta tumboni kwa kutumia matunda,
Zipo aina nyingi sana za vyakula/matunda ambavyo hutumika ktk kupunguza tatizo la mafuta tumboni,lkn leo nawaletea aina hizi saba za matunda ambayo tunatumia kila siku majumbani mwetu lkn hatujui kwa kiasi gani ni vizuri zaidi ktk kuondoa tatizo la mafuta mengi tumboni yanayopelekea mtu kua na kitambi iwe ni kwa wanawake au wanaume




1,,NYANYA

Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.

2,, TANGAWIZI

Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.





3,,JUISI YA LIMAU

Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.



4,,TIKITI MAJI

Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.



5,,TANGO

Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.

6,,PARACHICHI

Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba). Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.

Kula parachichi 1 kila siku.

7,,TUFAA

Kula tufaa maarufu sana kama 'apple' (epo) kunaweza kusaidia kupigana na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa mengi sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.

Hivyo kula tunda hili 1 kila siku asubuhi kupunguza shauku yako ya kutaka kula zaidi ndani ya hiyo siku


FAIDA 5 ZINAZOPATIKANA KWENYE MAJI YA NDIMU



Faida 5 za Kunywa Maji Yenye Ndimu

Faida 1. Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

Faida 2. Huboresha Kinga za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

 
Faida 3.Husaidia Unyonywaji wa Madini Mwilini

Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

Faida 4. Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicalsmwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

 Faida 5.Husaidia Kupunguza Hatari ya Kiharusi

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic (ischemic stroke) hasa kwa wanawake.


FUNGUA AKILI

Nimeipenda hiii kutoka kwa MASANJA MKANDAMIZAJI
_________________________________________
AKILI YAKO UTAJIRI WAKO:
_________________________________________
Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .
_________________________________________
Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.
__________________________________________
Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.
__________________________________________
Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!
__________________________________________
Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!
________________________________________
SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini
_________________________________________
MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!
_________________________________________
Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.
_________________________________________
KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.
________________________________________
Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka
__________________________________________
NI HAYO TU KWA LEO


MAMBO MATATU UNAYOWEZA KUYAPATA KWENYE UNGA WA MDALASINI

Mambo matatu unayoweza kuyapata kwenye unga wa mdalasini
_____________________________
Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza ladha nzuri katika kinywaji.
______________________________________
Mdalasini unaweza kutumika kuanzia magome, na mafuta yatokanayo na magome na kwenye majani.
__________________________________
Unapotumia unga wa magome yake huweza kupunguza matatizo mbalimbali kiafya ikiwa ni pamoja kusaidia kufanya uzazi kuwa karibu, ambapo kiungo hicho kitachanganywa na asali.
___________________________________
Pia matumizi ya mchanganyiko huo wa asali na mdalasini husaidia kuondosha lehemu (cholesterol) ndani ya mwilini
_________________________________________
Pia mdalasini na asali husaidia kutuliza mafua pamoja na kikohozi
Mbali na hayo, pia mdalasini husaidia kuzuia tatizo la gesi tumboni, kichefu chefu na kutapika.


USIPOTEZE MUDA IKIWA UMUHIMU WAKO UMESHAPOTEA

Inawezekana ulitumia muda mwingi sana kwa ajili yake lkn ameshindwa kuuona umuhimu wako kwa kurubunika na kitu kidogo sana,
________________________________________
aijalishi mlitoka mbali kiasi gani kinachoangaliwa hapo ni je amekuacha ktk mazingira gani?nini kilichosababisha akuache,
______________________________________
kipindi haupo nae alikuona wa thamani sana na akaweka ahadi nyingi moyoni kua akikupata utakua ndio mwanzo mzuri wa kuanzisha familia na wewe,mmebahatika kua pamoja anakuona wa kawaida,ameshakuzoea,hajali kitu,
______________________________________
ile thamani yako haioni tena,hajiulizi jinsi ambavyo anakudharau ww kuna wangapi huko nje wanapoteza time yao kukuwazia?najua utaumia lkn zingatia kitu kimoja,upendo wa kweli kwake usikufanye uwe mtumwa wa mapenzi,
_____________________________________
kama akishaanzisha dharau sema nae mara ya kwanza,ya pili,ya tatu na kuendelea ukiona haelewi anza kuinasua roho yako isije kuangamia kwa maumivu kipindi amekuacha,kwani yeye nani??
_________________________________________
walishapita wangapi kabla yake??ana nini kikubwa mno??ukishajiwekea maswali haya kichwani mwako huwezi kuyumba kamwe,


UPISHI WA CHAPATI ZA NYAMA

MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA .

Vipimo

Unga                                                            1 ½ vikombe vya chai

Mafuta                                                         ¼ kikombe cha chai

Chumvi                                                        ½ kijiko cha chai

Maji                                                              1 kikombe cha chai

Mafuta                                                          ½ kikombe cha chai


Mayai                                                            6 mayai

Manda nyembamba za mraba
(Spring roll pastries sheet)                              6


Nyama ya kusaga                                          ½ kilo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi    1 kijiko cha supu

Kotmiri iliyokatwakatwa                                 ½ kikombe

Chumvi                                                          kiasi

Pilipili manga                                                   ½ kijiko cha chai

Pilipili mbichi                                                     kiasi (ukipenda)

Bizari ya pilau ya unga                                     ½ kijiko cha chai.


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  



Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike

Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1.

Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe.

Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba .

Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha.


Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi.

Weka kwenye sahani tayari kuliwa


MOJA KATI YA DETOX NZURI YAKUPUNGUZA MWILI

Watu wengi wamekua wakilalamika kuhusu miili mikubwa,tumbo kubwa kiasi kwamba hawajui nini cha kufanya ili kukabiliana na hali hiyo
________________________________________
Nimekuletea moja kati ya detox nzuri na rahisi sana kuitengeneza nyumbani kwako
_________________________________________
Chukua tango moja
Spinach majani mawili
Ukikosa spinach tumia kabich
Embe moja na aple ya kijani moja
__________________________________________utatia kwenye blenda na maji kiasi kidogo yanayoweza kusagia detox yako
__________________________________________
Hakikisha inasagika na inakua nzito na usiitie sukari
______________________________________
Unaweza kunywa kabla hujaanza kula iwe breackfast,lunch hata dinner hakikisha unaanza kunywa detox alafu ndio unafatia kula chakula chako
_____________________________________
Kwa wale mnafanya diet nafkiri tumeelewana.


KUNA KIPINDI TUNATAKIWA TUKUBALI MATOKEO



Wakati mwingine hua tunajichosha kwa kujipa msongo wa mawazo kwa jambo la kujitakia

Unaweza ukaishi nae kwa salama na amani tuu hata miaka 20,lkn likaja kutokea lakutokea likasababisha mfarakano baina yenu

Hakuna hitimisho sahihi lililopo mbele yenu zaidi ya kuachana,je!utafosi uendelee nae kwa kisingizio kua tumetoka mbali?

Ndipo niliposema kujitafutia misongo ya mawazo isiyo na msingi,

Najua inauma na hasa kwa mliopendana kidhati lkn ikumbukwe kua kuna neno lisemwalo kua hakuna marefu yasiyo na ncha,,,au kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Ukikubaliana na haya utaamini ni kweli nisemacho ingawaje moyoni kinauma tena maumivu yake hayasemeki

Jaribu kuukubali ukweli kua yameshatokea

Jaribu kuupa moyo nafasi nyingine huenda ni bora pia kuliko ulipotokea

Kila likuepukalo lina heri ndani yake

Kuforce sana vitu visivyowezekana kunaweza kufupisha maisha yako

Sisemi umuache kirahisi,jaribu kupambana ili uwe nae,lkn kama ikishindikana jifunze kuukubali ukweli kua haiwezekani na upige moyo konde kuanza kupiga hatua mpya itayokusogeza mahali pengine


#Achaibakistory

Monday, July 10, 2017

ZIJUE FAIDA TISA ZINAZOPATIKANA KWENYE MCHAICHAI





1. Kuzuia kutapika

2. Kutuliza maumivu ya tumbo

3. Kupunguza makali ya homa.

4. Msaada kwa wenye tatizo la  baridi yabisi,

5. Husaidia  kusafisha figo

6. Huzuia tatizo la tumbo kuunguruma
7. Husaidia uyeyushaji wa chakula

8. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na maumivu mbalimbali ya mwilini.

9. Husaidia kupunguza maumivu kwa kinamama wakati wa hedhi 


JIFUNZE KULIEPUKA HILI KTK MAHUSIANO YAKO

Adui mkubwa wa mahusiano yako ni uyu apa👉MAZOEA,,,ukiishi kimazoea mtaachana kwa sababu zisizo na msingi,ili udumu nae jifunze kumuona mpya kila siku,usiuruhusu moyo wako ujenge kitu kinaitwa MAZOEA,mazoea yanasababisha umuone wa kawaida uanze kupunguza upendo,mazoea yanasababisha umdharau kwa kuona kwamba nimeshamzoea ata akiniacha poa tuu,mazoea hayo hayo yanakufanya uishushe thamani yako hata kama alikua anakupenda kiasi gani,,mnajua kwa nn wenzetu wanadumu sana tofauti na couple za africa??afrika tumejizoesha vibaya kwa kuweka mazoea mbele,,wenzetu wanajua jinsi ya kuishi ili kila siku mtu amuone mwenzie mpya,end of the day utaskia wenzetu wale wanaishi kizungu,,sio kizungu ni wewe mwenyewe kuucontrol moyo wako kwa kuweka kitu kinaitwa NEW,, muone mpya kila siku utaamini nnalosema,au kama hutaki ishi nae kimazoea halafu utakuja kuhakikisha kweli msemo wangu una maana kubwa,, 


Sunday, July 9, 2017

EPUKA KUONESHA MACHUNGU YAKO YA MOYONI MBELE ZA WATU




Jifunze kuficha machungu yako mbele za watu,   kwa sababu  huwezi kumjua yupi rafiki na yupi  adui      wapo wataohuzunika na wewe lkn wapo ambao hupenda kukuona ukiwa na huzuni ata milele        jiepushe kuwapa faida maadui zako



Fish balls

FISH BALLS MAHITAJI Tuna vibati viwili (au samaki asiekuwa na miba wa kiasi) Cheese 3/4 cup (tea cup) iloparwa Carrot ndogo 1 (iloparwa ...